.
Wednesday, September 30, 2009
Wasanii wa filamu waicharukia BASATA!
Wadau pamoja na wasanii wa filamu nchini leo (Ijumaa) wanatarajia kukutana katika Uwanja wa Leaders Club ili kupinga uamuzi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kukataa kusajili chama chao kwa kile kilichodaiwa kuwa, nao walikuwa na lengo la kuanzisha chombo kama hicho.
Wasanii hao waliamua kuanzisha chama hicho walichokiita Tanzania Film Federation (TAFF) kwa lengo la kuwaunganisha na kutetea haki zao lakini BASATA waliwawekea ‘kauzibe’ hivyo kukubaliana kukutana ili kutafakari cha kufanya.
Wakiongea na Ijumaa juzi katika nyakati tofauti, wasanii hao walisema kuwa wamelishangaa sana Baraza hilo kwa kuwakwamisha katika jitihada zao za kutaka kuunda chombo cha kuwalea pamoja hivyo wameandaa mkutano huo ambao utawakutanisha wasanii wote nchini ili kuweka mikakati itakayowasaidia.
“Tumeandaa mkutano unaotarajia kufanyika siku ya Ijumaa (leo) kuanzia saa nane ili kuhakikisha tunapanga mikakati ya pamoja ili kuhakikisha tunakuwa kitu kimoja bila kuyumbishwa na watu wachache wanaotumia BASATA,” alisema Chekibudi.
Aidha, Ijumaa lilibahatika kuongea na mmoja wa maafisa wa BASATA aliyetambulika kwa jina la Omary Mayanga ambaye alikiri Baraza hilo kukataa kusajili chama hicho cha wasanii lakini kwa maelezo zaidi akamtaka mwandishi kuwasiliana na Katibu Mkuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment