.

.

Friday, February 19, 2016

Mask ya boga kwa wenye chunusi

Nilishaandika sana urembo unaohusu chunusi lakini kila kukicha napata ujumbe unaotaka kujua tiba ya chunusi, leo nakuletea maski ya boga ambayo ni nzuri kwa kutibu chunusi.
 Chukua boga lipike liive kisha chukua kikijiko kimoja  1 cha boga
  Kijiko kimoja cha asali 1
Robo kijiko cha mdarasini

JINSI YA KUFANYA
 Chukua kila kipimo weka kwenye kibakuli kisha changanya kwa pamoja upate mkorogo mmoja.
Baada ya hapo paka kwenye uso taratibu mpaka usambae uso mzima.
Acha kwa muda wa dakika 5 kisha osha na maji ya vuguvugu.

Kumbuka: Kama ngozi yako ina alegi yoyote usitumie, kama ngozi yako ni ya kawaida tumia maski hii Itakusaidia kuondoa chunusi na kukufanya utelezee.