Mask ya boga kwa wenye chunusi
Nilishaandika sana urembo unaohusu chunusi lakini kila kukicha
napata ujumbe unaotaka kujua tiba ya chunusi, leo nakuletea maski ya boga
ambayo ni nzuri kwa kutibu chunusi.
Chukua boga lipike
liive kisha chukua kikijiko kimoja 1 cha
boga
Kijiko kimoja cha
asali 1
Robo kijiko cha mdarasini
JINSI YA KUFANYA
Chukua kila kipimo
weka kwenye kibakuli kisha changanya kwa pamoja upate mkorogo mmoja.
Baada ya hapo paka kwenye uso taratibu mpaka usambae uso
mzima.
Acha kwa muda wa dakika 5 kisha osha na maji ya vuguvugu.
Kumbuka: Kama
ngozi yako ina alegi yoyote usitumie, kama ngozi yako ni ya kawaida tumia maski
hii Itakusaidia kuondoa chunusi na kukufanya utelezee.
No comments:
Post a Comment