.

.

Thursday, April 29, 2010

Send off ya Jose Njunwa

Hapa amepiga picha na mheshimiwa waziri mkuu mstaafu

Akijiandaa kupeleka keki kwa wakwe zake
Akielekea kukata keki


Jose akiwa na mume wake na matroni wake




Jose na ndugu zake kama tunavyowaona walikuwa katika furaha ,lakini pia walipata majonzi kwa kumbukumbu ya wazazi wao waliotangulia mbele ya haki mungu awalaze pema peponi, kwani ilikuwa ni siku ambayo hakika wangefurahi kuona sherehe ya mtoto wao



Saturday, April 17, 2010

Baada ya shughuri zote Tukafunguliwa muziki na Mama kijacho tukajumuika wote

Hawa walikuwa wakibadirishana mawazo
Jack naye aliserebuka kiaina
Mama kijacho kafurahi huyo
muziki alicheza sana tukadhani atajifungua siku hiyo, jamani ilikuwa ni furaha
Mama kijacho akifungua muziki na Johari
Hawa wakanogewa muziki na kuoneshana miguu wakilingishiana nani zaidi
Fide akisaka lumba kwa madaha na kinywaji chake
Hapa umekolea kweli kila mtu na zake staili
Hapa mama kijacho wala hakumbuki nyumbani kwani ukumbini kulimtoshereza kwa kila kitu

Keki ya Kyalaa na Melisa inaendelea kuliwa

Kyalaa akipewa dola na dada mpendwa Devotaa kama zawadi ya kumpongeza kufikisha miaka kadhaa
Hapa akipewa dhawadi na mpenzi wake
Hapa akimlisha Keki dada yake Shamimu
Na huyu ni dada yake Mery Raphael akimlisha keki
Mama kijacho naye hakuwa mbali katika keki,kama tunavyomuona

Baada ya baby shower kukawa na Birthday ya Kyalaa na Melisa

Melisa na Kyalaa walianza kupuliza mishumaa
Sister Doi nikawa wa kwanza kulishwa keki kwa jinsi wanavyonimind

Ant Ezekiel alikuwa Mc wa shughuri na ndiye aliwawashia mishumaa kama mnavyomuona

birthday nayo ilichangamsha tuliamua kufanya sherehe zote kwa mpigo kweli tulifurahi sana

zawadi zinaendelea

Fide alimletea mama kijacho kinywaji kama tunavyomuona
waandaaji wa shughuri nao na zawadi yao

rafiki wa mama kijacho alikuja kumuwakirisha Lily wa mambo hayo na zawadi yake

Friday, April 16, 2010

Zawadi zikaanza

Jackqueline Patrick akienda kutoa zawadi kaanza kwa ku hug , mama kijacho kafurahi
Akaanza kutoa zawadi zake sasa
kabla ya kumkabidhi si mapozi ya kimiss yakachukua nafasi baada tu ya kuona kamera

Huyu ni Melisa a.k.a Maarufu kwa wakati wake naye alikuwepo
kama mnavyomuona naye alikuwa na zawadi zake

Zamu ya Bi dada Mery Raph, yeye alikuwa na furaha kama tunavyomuona
Zawadi zake zilikuwa ni adimu kwani alitoa zawadi ya kipekee kwa kijacho

Neema Chande yeye alibeba Pampasi kilo Hamsini mama Kijacho anunui mpaka Kijacho anaacha anajitambua na kuomba poti
Zamu ya Johari yeye aliingia kwa mbwembwe za muziki na zawadi yake kama mnavyoiona

Sauda mwilima naye alikuwepo kama kawa na zawadi yake

Jackline Woper alikuwepo pia
Dada Mkubwa Devotaa yeye alitoa zawadi kama dada kwa alimpatia madola mdogo wake pamoja na zawadi nadhani picha zinaonesha



Mama kijacho akiwa katika kocho akisubiri wageni waalikwa jamani tunamuombea ajifungue salama, amina atapata mtoto wa kike.