.

.

Thursday, August 12, 2010

tunaendelea kujidai

Baada ya kurudi home mwanangu huwa ananikimbilia kuni hugh kama hivi siku hiyo nilijisikia kumpiga picha

Nimerudi jamani nilikuwa kando kidogo

Kama kawa tunajidai na mwanangu, jamani msituchoke hatuna albamu hii ndio albamu yetu
my Baby Mzuri katika pozi
Mimi na Baby wangu nikitoka kazini huwa anakuja kudeka kidogo kama mnavyomuona
Hapa nilikuwa Club Bilicanasi kwenye ukumbi wa Much More nilipoalikwa MTVBASE

Wednesday, July 28, 2010

Nikaalikwa kichen Paty na Dotnatha

Dot akiwa na furaha pamoja na wasanii wake waliomuunga mkono
maswahiba wawili, Mona na Thea
Hapa wanachama wenzake wanamzawadia
Sisterdoi na Mdogo wangu Achi tuliongozana mpaka kunako sherehe hiyo
Hapa nikiwa na mdogo wangu Lulu
Mama na mwana nao walikuwepo
Baada ya zawadi wanachama wakaendelea kujimwaga

Siku ya Production Jumanne

Sister Doi na Graphic Di signer wa Gazeti ninalofanyia kazi Nasra Nasoro, nyuma yetu ni kaka Mchele akipita kukagua gazeti kwa ajili ya kuandaa oda, siku hii huwa ni ngumu kwangu kwani nakuwa bize kinoma, hata simu huwa sipendi kupokea kwakweli nakuwa siriasi kwenye kazi
Mpiga picha wetu Walter Maleko aliamua kutufotoa mimi na Nasra tukiwa mbioni kumalizia kazi

Wednesday, July 21, 2010

Mimi na mwanangu tulipokutana baada ya miezi kadhaa alipokuwa kwa bibi yake

Hapa mzuri akimnongoneza jambo wake Hamidu a.k.a Papaa
Mzuri na mama yake wakiwa happy, pozi la maana hilo nawe chukua
Mzuri katika pozi, mh haya ni mapozi ya mama yake si mchezo
Hapa ameona avae kiremba cha mama yake
Alikuwa akivua viatu ili akae vizuri kwenye kiti
Hapa mzuri akiwa na mama yake, katika pozi la picha

Friday, July 2, 2010

Friend of mine Baba Ally akiwa kazini

Huyu ni Amran Kaima a.k.a Baba Ally akiwa kazini, hapa anasikiliza Cd ya ushahidi wa Habari, ukitaka kumjua zaidi gonga kwenye Blog yake inaitwa Zekaima.blogspot.com

Usafi Day in the ofisi..Global Publishers

Lea Kweka naye alikuwa akisafisha vioo kama tunavyomuona
Wadada tuliamua kufanya usafi wa jumla siku hii ya Ijumaa, Hawa ni Edna, Abby na Groly
Sister Doi nikisafisha meza na Dada Grace pembeni yangu
Naila naye alikuwa akisafisha kama tunavyomuona

Hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Dada Dotnatha na Ant Latifa na Sharom

Align Center Sharom akijiimbia siku ya kuzaliwa kwake
Da Jen naye alikuwepo
Eva katika pozi naye alishiriki
Natasha akilishwa keki na Dotnatha
Hapa waliozaliwa siku hiyo wote wanakata keki
Na hii nayo ni ya kukata keki
Hapa wakilishana Keki aliyeshika Uma ni Anti Latifa na aliyemeza ni Dotnatha
Ant Latifa Katika pozi
Mama Sofia Bariagati katika pozi naye alikuwepo
Monalisa naye alikuwepo
Sister Doi nilikuwepo kama kawa, hapa alikuwa akilishwa keki mama Sharom, Shamim

Saturday, June 19, 2010

LILY WA MAMBO HAYO ALIPOMFANYIA MWANAYE SHEREHE YA KUZALIWA

Rafiki yangu Shamim naye alikuwepo katika sherehe hiyo
Sister Doi nikilishwa keki ilikuwa tamu kinoma
Hapa akikata keki
Hapa Rahimu anamlisha mama yake keki
Mama anamshukuru kwa kumpa busu zito
Keki hii ilikuwa tamu kwani nami niliionja
Hapa wakiwa katika pozi la furaha

Thursday, June 17, 2010

Dont mess with an Angle inavyoendelea


Jumatatu..
Mayita Juan anaendelea kumlalamikia Miguel kuwa alitaka kumuua mama yake.
Sehemu ya 36:
Mayita anamlalamikia Juan Miguel kuwa alitaka kumuua mama yake, maneno madogo ambayo Viviana alimjaza, Miguel anamwambia kuwa sio ukweli kwasababu mama yake kwa sasa yuko mbinguni, Mayita hakubariani na baba yake anasisitiza kuwa mama yake hivi karibuni atarudi nyumbani kwao. Juan Miguel anakiri kwa Vicente kwamba yeye ndio alitaka kuvunja penzi lake kwasababu ya ajari aliyoisababisha kwa dada yake ambaye aliumia sana usoni, Vicent anapata mshtuko anaposikia. Marichoy anapewa karatasi za kuandaa talaka yake, na mtu anayemshawishi kufanya hivyo ni Adrian. Rocio anakuwa amelala usingizi, Vicente anagundua kilichotokea usoni kwa mpenzi wake, Racio anapoamka na kumkuta Vicente anamuomba aondoke kwani hakutaka amuone, Vicente anamwambia Racio kwamba wala hajali na kujitolea kumsaidia.
Jumanne
Sehemu ya 37:
Candelaria anapata maumivu makali na kuzimia.
Candelaria anahisi maumivu makali, anajaribu kupuuza lakini mwisho wa siku anazimia, watu wanakuja kumsaidia. Stephanie anamrubuni Juan Miguel, anamwambia kuwa atamsaidia kurudisha penzi la Mayita iwapo atamuoa yeye.
Viviana anaendelea kutalii nyumbani kwa San Román, ambaye ametoka na Stephanie anayepoteza muda waki akidhani atampata Juan Miguel,wakati anaye wa kwake.
Candelaria anawasiliana na Vencindad, anamwambia kuwa alisikia kizunguzungu na kuzimia,Marichuy akiwa na wasiwasi anafanikiwa kumsaidia 'Candida'.
Marichuy anakwenda kumtenbelea Vicente na Rocio huko Hospitali,akajaribu kwenda kitandani kwake lakini rafiki yake anamzuia, akajikuta anagundua kuwa ana kizunguzungu.

Jumatano - Juan Miguel na Marichuy wanajadiriana huko Hospitali. Juan Miguel, Rocio na Marichuy wanakutana Hospital, Miguel anamuomba Marichuy akubari pesa anazompatia, akakataa na kumwambia kuwa walioana kwa usiku mmoja tu. Juan Miguel hakubariana naye anamwambia kuwa anataka kumsaidia. Marichuy anamwambia amuache aondoke, akasema kuwa atarudia kumuoa mara nyingi zaidi hata iwe mara elfu moja na kumwambia kuwa wao wako kwenye mapenzi, akawa anamuinamia akitaka kumbusu mpaka pale Cecilia alipofika na kuvuja maongezi yao. Marichuy anaondoka wodini Juan Miguel anamfuata, akamlalamikia kuwa kwanini hakumwambia Candelaria yuko hospitali hiyo hiyo, akajibu kuwa hakuhitaji kutoa ufafanuzi na kumuhakikishia kuwa hataki pesa yake, bila kutarajia Marichuy anaanguka mikononi mwa Juan Miguel. Candelaria anamuuliza Marichuy anajisikiaje?, anasema kuwa anasikia kizunguzungu na kukosa nguvu, Candelaria anamjibu kuwa mara nyingi hali hiyo huwa inamtokea mwanamke mjamzito Marichuy anashtuka baada ya kusikia vile.

Juan Miguel anapandishwa kizimbani kwa kesi ya kumbaka Marichuy!
Leo tunamuona Juan Miguel ametinga kizimbani baada ya kushtakiwa na Marichuy. Marichuy anafika mahakamani kutoa ushahidi wa kubakwa na jinsi alivyougulia maumivu ya kitendo hicho kwa miaka kadhaa, Mr. del Villar anamuuliza swali na kutaka kujua ni kitu gani kilitokea, akisisitiza kujua kama kweli Juan Miguel alimvamia, Marichuy anajibu kuwa mtu aliyembaka si mrefu na mwenye nguvu. Baada ya majibu hayo Juan Miguel anaondoka eneo la mahakama akiwa na mawakiri wawili, akiwa na wasiwasi wa kuanguka kutokana na mawazo kuwa kama atapotea hatokaa ataonekana mwenye hatia hatokaa akasamehewa na Mayita waka Marichuy.

Ijumaa: Amador anamwambia Marichuy kwamba atamfanya awe maarufu.
Mahakama inampatia uhuru Juan Miguel, hivyo anaweza kukaa na Mayita pia ikaifunga kesi kitendo ambacho kilimpatia furaha Dr. San Román. Leticia anamwambia Viviana kuwa mume wake anaye mwanamke mwingine,Viviana akajikuta anastushwa na habari hizo. Amador anamwambia Marichuy kuwa yeye ni almasi chafu lakini yeye atahakikisha anamsafisha, Marichuy anachukia baada ya kuambiwa hivyo lakini akamwambia kuwa baadae atakuja kuwa wa kimataifa zaidi. Onelia anataka kumchukua Mayita akamlee lakini Juan Miguel anamwambia kuwa mtoto wake haendi popote, kitendo hicho kinamkera Onelia ambaye anaamua kumpiga kibao Miguuel.Je nini kitaendelea usikose wiki ijayo.