.

.

Thursday, June 17, 2010

Dont mess with an Angle inavyoendelea


Jumatatu..
Mayita Juan anaendelea kumlalamikia Miguel kuwa alitaka kumuua mama yake.
Sehemu ya 36:
Mayita anamlalamikia Juan Miguel kuwa alitaka kumuua mama yake, maneno madogo ambayo Viviana alimjaza, Miguel anamwambia kuwa sio ukweli kwasababu mama yake kwa sasa yuko mbinguni, Mayita hakubariani na baba yake anasisitiza kuwa mama yake hivi karibuni atarudi nyumbani kwao. Juan Miguel anakiri kwa Vicente kwamba yeye ndio alitaka kuvunja penzi lake kwasababu ya ajari aliyoisababisha kwa dada yake ambaye aliumia sana usoni, Vicent anapata mshtuko anaposikia. Marichoy anapewa karatasi za kuandaa talaka yake, na mtu anayemshawishi kufanya hivyo ni Adrian. Rocio anakuwa amelala usingizi, Vicente anagundua kilichotokea usoni kwa mpenzi wake, Racio anapoamka na kumkuta Vicente anamuomba aondoke kwani hakutaka amuone, Vicente anamwambia Racio kwamba wala hajali na kujitolea kumsaidia.
Jumanne
Sehemu ya 37:
Candelaria anapata maumivu makali na kuzimia.
Candelaria anahisi maumivu makali, anajaribu kupuuza lakini mwisho wa siku anazimia, watu wanakuja kumsaidia. Stephanie anamrubuni Juan Miguel, anamwambia kuwa atamsaidia kurudisha penzi la Mayita iwapo atamuoa yeye.
Viviana anaendelea kutalii nyumbani kwa San Román, ambaye ametoka na Stephanie anayepoteza muda waki akidhani atampata Juan Miguel,wakati anaye wa kwake.
Candelaria anawasiliana na Vencindad, anamwambia kuwa alisikia kizunguzungu na kuzimia,Marichuy akiwa na wasiwasi anafanikiwa kumsaidia 'Candida'.
Marichuy anakwenda kumtenbelea Vicente na Rocio huko Hospitali,akajaribu kwenda kitandani kwake lakini rafiki yake anamzuia, akajikuta anagundua kuwa ana kizunguzungu.

Jumatano - Juan Miguel na Marichuy wanajadiriana huko Hospitali. Juan Miguel, Rocio na Marichuy wanakutana Hospital, Miguel anamuomba Marichuy akubari pesa anazompatia, akakataa na kumwambia kuwa walioana kwa usiku mmoja tu. Juan Miguel hakubariana naye anamwambia kuwa anataka kumsaidia. Marichuy anamwambia amuache aondoke, akasema kuwa atarudia kumuoa mara nyingi zaidi hata iwe mara elfu moja na kumwambia kuwa wao wako kwenye mapenzi, akawa anamuinamia akitaka kumbusu mpaka pale Cecilia alipofika na kuvuja maongezi yao. Marichuy anaondoka wodini Juan Miguel anamfuata, akamlalamikia kuwa kwanini hakumwambia Candelaria yuko hospitali hiyo hiyo, akajibu kuwa hakuhitaji kutoa ufafanuzi na kumuhakikishia kuwa hataki pesa yake, bila kutarajia Marichuy anaanguka mikononi mwa Juan Miguel. Candelaria anamuuliza Marichuy anajisikiaje?, anasema kuwa anasikia kizunguzungu na kukosa nguvu, Candelaria anamjibu kuwa mara nyingi hali hiyo huwa inamtokea mwanamke mjamzito Marichuy anashtuka baada ya kusikia vile.

Juan Miguel anapandishwa kizimbani kwa kesi ya kumbaka Marichuy!
Leo tunamuona Juan Miguel ametinga kizimbani baada ya kushtakiwa na Marichuy. Marichuy anafika mahakamani kutoa ushahidi wa kubakwa na jinsi alivyougulia maumivu ya kitendo hicho kwa miaka kadhaa, Mr. del Villar anamuuliza swali na kutaka kujua ni kitu gani kilitokea, akisisitiza kujua kama kweli Juan Miguel alimvamia, Marichuy anajibu kuwa mtu aliyembaka si mrefu na mwenye nguvu. Baada ya majibu hayo Juan Miguel anaondoka eneo la mahakama akiwa na mawakiri wawili, akiwa na wasiwasi wa kuanguka kutokana na mawazo kuwa kama atapotea hatokaa ataonekana mwenye hatia hatokaa akasamehewa na Mayita waka Marichuy.

Ijumaa: Amador anamwambia Marichuy kwamba atamfanya awe maarufu.
Mahakama inampatia uhuru Juan Miguel, hivyo anaweza kukaa na Mayita pia ikaifunga kesi kitendo ambacho kilimpatia furaha Dr. San Román. Leticia anamwambia Viviana kuwa mume wake anaye mwanamke mwingine,Viviana akajikuta anastushwa na habari hizo. Amador anamwambia Marichuy kuwa yeye ni almasi chafu lakini yeye atahakikisha anamsafisha, Marichuy anachukia baada ya kuambiwa hivyo lakini akamwambia kuwa baadae atakuja kuwa wa kimataifa zaidi. Onelia anataka kumchukua Mayita akamlee lakini Juan Miguel anamwambia kuwa mtoto wake haendi popote, kitendo hicho kinamkera Onelia ambaye anaamua kumpiga kibao Miguuel.Je nini kitaendelea usikose wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment