.
Wednesday, September 30, 2009
Fat Joe amtupia matusi 50 Cent.
Wasanii wa muziki wa Hip Hop wa Marekani Fat Joe na 50cent wameingia katika bifu kali kitendo kilichopelekea Fat Joe kumtolea maneno machafu 50 cent kama majibu baada ya kuikashfu albamu yake na kudai kuwa albamu aliyoitoa inamsababishia kuumwa sana na kukimbizwa hospitali.
Hivi karibuni msanii huyo kutokea kundi la G unit alilalamika kukimbizwa hospitali baada ya kusikiliza Albamu ya Fat Joe iliyoitwa J.O.S.E. Part II.
Kwa mujibu wa mtandao wa Fif,umedai kuwa albamu hiyo ndio imesababisha hasa kuumwa kwa msanii huyo baada ya kuisikiliza na kuangua kilio.
Akijibu msanii Fat Joe ambaye alikuwa ameng'aka alitoa matusi makali na kusema kuwa kama kweli ni albamu yake imesababisha hivyo basi ana uchizi na ameenda mbali katika utani!
Mbali na mtandao huo kusema hivyo pia habari kutoka kituo cha polisi cha Manhattan zilidai kuwa msanii huyo alizimia na kukimbizwa hospitali baada ya kusikiliza albamu ya Fat ambayo ilionekana kusababisha kutokea kwa hali hiyo.
Kuonesha ukweli wa jambo hilo mtandao wa Sohh umeonesha video ya msanii huyo akiwa na bandeji usoni kwake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment