.
Wednesday, September 30, 2009
Isabela akimbilia kwa Gaetana!
Wiki iliyopita katika tamthilia tumeona mengi ikiwa ni pamoja na Angela anakosa furaha pale anapokumbuka wimbo aliomchagulia baba yake.
Isabel anasafiri na kwenda Las Cruces, ambako atakutana moja kwa moja na Cantalicia.
Gaetana anamuota Cerinza akiumwa sana na anamuona vile anavyoteseka.
Antonio anagundua mambo ya ajabu yaliyomzunguka Salvador.
Abigail anapokea habari mbaya ya kifo cha mume wake na kwenda kutembelea kabuli lake.
nini kitatokea?Endelea kusoma…
Valeria anakiri kwa Simon kwamba siku zote anampenda Pedro José. Huku kwa akina
Isabel na Salvador baada ya kubaini ukweli kutoka kwa Cantalicia wanaamua kumsaidia kiasi Fulani cha pesa Cantalicia na Monchito.
Rebeca anakuwa hana muda wa kuandaa mkutano na Elizabeth na kuunda chuki kisha kujitetea kwa kutoa maoni kwa Salvador.
Kubwa kabisa, anasisitiza kwamba Isabela hatakiwi kuaminika kwasababu anashawishiwa kwamba kuna kitu anachokificha.
Isabel baada ya kuona mambo yamemuwia magumu anaamua kumtembelea Gaetana. Hata hivyo, mtabiri huyo anakuwa hayuko tayari kumpatia msaada na kukataa kisha akamuweka wazi na kumwambia kuwa inawezekana Peter Joseph na mume wake ambaye ni Salvador ni mtu mmoja.
Je Isabela atafanya nini baada ya kupewa live na Gaetana? Usikose uhondo wa tamthilia hii ambayo inaelekea ukingoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment