.
Wednesday, September 30, 2009
TID, Banana waitosa Twanga!
Vinara wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini Khaleed Mohamed a.k.a TID na Banana Zahir Zorro waliwaacha watu hoi baada ya kugoma kupanda katika jukwaa la Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ ambayo ipo chini ya Kampuni ya ASET inayomilikiwa na Asha Baraka.
Tukio hilo lililopokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki, lilichukua nafasi wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo bendi hiyo hufanya vitu vyake kila Jumamosi.
TID na Banana walionekana kuwepo ukumbini humo wakifuatilia kwa makini onesho hilo huku mara nyingi wanamuziki wa bendi hiyo wakiwarusha kama ishara ya kutambua uwepo wao.
Hata hivyo baadaye, wanamuziki wa bendi mbalimbali walipotakiwa kupanda jukwaani kwa ajili ya kuwasalimia mashabiki, wasanii hao hawakuonekana!
“Naam, wasanii huwa tunasalimiana kisanii, hivyo nawaomba wasanii wote ambao mpo humu ndani, mje kuwasalimia mashabiki....” Charles Gabriel a.k.a Charles Baba alisikika akisema.
Wasanii wengine wakiwemo Badi Bakule na Jua Kali wa Tanzania One Theather ‘T Respect’ walipanda jukwaani na kukonga nyoyo za mashabiki, lakini mastaa hao wa Bongo Fleva hawakutia timu.
“Wapi Banana na TID, tunawasubiri mbele jamani, njoeni...njoeni jamani...” Charles Baba alizidi kuwaomba wapande lakini hawakutokea.
Baada ya kuitwa kwa muda mrefu na kuonekana kutokuwa na mpango wa kupanda jukaani, Badi Bakule na Jua Kali kwa nyakati tofauti waliwasha moto ambapo waliwakuna sana mashabiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment