.
Wednesday, September 30, 2009
RAY C MBARONI
Msanii wa kike anayesumbua katika muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila a.k.a Ray C hivi karibuni alijikuta akitiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa madai ya kumtapeli promota wake aliyetambulika kwa jina la David Masatu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Ray C alinaswa mwishoni mwa wiki iliyopita na ‘Vijana wa Mwema’ wa kituo hicho akidaiwa kutia ndani kiasi cha shilingi 600,000 za promota huyo alizopewa ili ikafanye shoo mkoani Mwanza.
Ilidaiwa kuwa, baada ya mwanadada huyo kupewa mkwanja huo kama ‘advansi’ kufuatia makubaliano ya kufanya shoo mbili kwa shilingi 1,200,000, siku ya kukwea pia kuelekea Rock City ilipowadia, alikuwa hapatikani hewani.
Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya promotoa huyo kubaini kuwa kaingizwa mjini alikwenda katika kituo cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia Ray C kesi yenye jalada namba OB/RB/17123/09, KUTAPELI.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita (Jumapili) msanii huyo alinaswa na polisi kisha kufikishwa katika kituo hicho na kuhojiwa kwa saa kadhaa.
Baada ya kufikishwa kituoni hapo, msanii huyo aliomba ishu isiende mbali na kuahidi kurudisha nusu ya pesa alizopewa (300,000) huku akiomba apewe siku 14 kutekeleza hilo ambapo alikubaliwa kisha kujidhamini mwenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment