.

.

Tuesday, September 15, 2009

Huu ndio mwisho wa wapendanao Amina na mpakanjia





ENZI ZA MAISHA YA
UPENDO YA AMINA NA
MEDDY MPAKANJIA

Maisha ya
m a r e h e m u
A m i n a
Chifupa na
M o h a m e d
Mkapanjia a.k.a Meddy
yalikuwa ya upendo
wa dhati ndiyo maana
watu wengi walikuwa
wakiyatafsiri kuwa ni ya
kutegemeana. Kupendana
kwao huko kumezua
minong’ono kwa watu
mbalimbali wakidai huenda
mkewe amemchukua.
Hata hivyo, inabaki kuwa
kazi ya Mungu haina
makosa.
Historia yao kwa ufupi:
Amina alizaliwa 1981-2007
alikufa akiwa na miaka (26)
Meddy alizaliwa mwaka
1972-2009 amekufa akiwa
na miaka (37)
Historia ya ndoa yao:
Walioana mwaka 2001
Amina akiwa ni mjamzito
wa miezi saba.
Walijaaliwa kupata mtoto
wao wa kwanza Rahman
‘Ramanino’ mwaka 2002.
Baada ya hapo mapenzi
yao yalikuwa motomoto
walikuwa wanandoa
waliofuatana kila kona hasa
kwenye kumbi za starehe.
Amina alikuwa ni
mshereheshaji wa shughuli
‘MC’ na pale alipokuwa
akiwajibika mume wake
alikuwa pembeni yake,
hakika walipendana na
ndiyo maana baada ya kifo
cha Amina Chifupa afya ya
Mpakanjia ilianza kuwa tete
kwani alianza kuandamwa
na msongo wa mawazo na
maradhi kadhaa kutokana
na upweke wa kuondokewa
na kipenzi chake.
Amina na Mpakanjia wote
walifia katika Hospitali
ya Jeshi ya Lugalo baada
ya kulazwa kwa muda
mchache huku Meddy
akidaiwa kufa kwa Homa
ya matumbo ‘Typhoid’
na Amina arifariki kwa
matatizo ya msongo wa
mawazo.
Mwisho naweza kusema
kuwa maisha yao yalikuwa
ya upendo na wamemuacha
mtoto wao Rahmanino
katika hali ya uzuni. Mungu
awalaze pema peponi.
Amini.
***
MEDDY MPAKANJIA:
ILIKUWA LAZIMA AFE
Mohamed Mpakanjia
a.k.a Meddy Mpakanjia,
inaonekana ilikuwa lazima
afe kutokana na ‘midomo’
ya watu ambapo tangu kifo
cha mkewe, Amina wamekuwa wakisema
hata yeye asingeishi sana.
Mbali na uchuro huo, taarifa za uvumi
wa kifo chake zilizokuwa zikienezwa kwa
njia ya mitandao na vyombo vya habari,
ilikuwa ikitikisa uhai wake kwa muda
mrefu.
Kwa mara ya kwanza, Mpakanjia
alizushiwa kifo mwezi Agosti mwaka
2007 baada ya kuugua na kulazwa katika
Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) Lugalo, kisha vyombo
vya habari vikaripoti kuwa alikuwa
ameaga dunia.
Tangu kipindi hicho, Mpakanjia alikuwa
akidai kushindwa kuzuia hisia zake za
kumpenda mkewe aliyemuacha wakiwa
bado wana pendo la dhati na kusababisha
kuzibandua picha zote za Amina
zilizokuwa ukutani mwa nyumba yake
kwa lengo la kupoteza kumbukumbu.
Wachunguzi wa masuala ya saikolojia
walisema kuwa, Mpakanjia aliathirika
kisaikoloji na kujikuta anakuwa na
msongo wa mawazo kutokana na kuishi
akiwa mpweke. Aidha, wataalam wa
maisha wanadai kuwa, mara nyingi mke
akitangulia kufa, mume naye haishi miaka mingi

No comments:

Post a Comment