.

.

Wednesday, September 30, 2009

Ndoa kuota mbawa!


Ndoa ya mwanadada Kylie Minogue huenda ikaota mbawa kabla ya kuolewa baada ya mchumba wake ambaye ni mdogo kiumri kughairi mambo ya kufunga ndoa.
Mchumba huyo alipokuwa akiongelea mambo ya chumbani alimsifia sana Minogue lakini alisema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuoa kwani bado ana mambo mengi ya kufanya,lakini anampenda sana mpenzi huyo na anaimani huenda wakapata baby mzuri sana kutokana na sura zao siku watakayoamua kuzaa...

Fat Joe amtupia matusi 50 Cent.


Wasanii wa muziki wa Hip Hop wa Marekani Fat Joe na 50cent wameingia katika bifu kali kitendo kilichopelekea Fat Joe kumtolea maneno machafu 50 cent kama majibu baada ya kuikashfu albamu yake na kudai kuwa albamu aliyoitoa inamsababishia kuumwa sana na kukimbizwa hospitali.
Hivi karibuni msanii huyo kutokea kundi la G unit alilalamika kukimbizwa hospitali baada ya kusikiliza Albamu ya Fat Joe iliyoitwa J.O.S.E. Part II.
Kwa mujibu wa mtandao wa Fif,umedai kuwa albamu hiyo ndio imesababisha hasa kuumwa kwa msanii huyo baada ya kuisikiliza na kuangua kilio.
Akijibu msanii Fat Joe ambaye alikuwa ameng'aka alitoa matusi makali na kusema kuwa kama kweli ni albamu yake imesababisha hivyo basi ana uchizi na ameenda mbali katika utani!
Mbali na mtandao huo kusema hivyo pia habari kutoka kituo cha polisi cha Manhattan zilidai kuwa msanii huyo alizimia na kukimbizwa hospitali baada ya kusikiliza albamu ya Fat ambayo ilionekana kusababisha kutokea kwa hali hiyo.
Kuonesha ukweli wa jambo hilo mtandao wa Sohh umeonesha video ya msanii huyo akiwa na bandeji usoni kwake.

Eti Hannington ananuka kikwapa!


Kuna sababu nyingi zinaweza kumtoa mshiriki katika mpambano huu lakini hili la mshirikiti kutoka Uganda, Hannington kudaiwa kuwa anatema harumu mbaya kutoka mwilini mwake, huenda likamkoseha kabisa matumaini ya kundelea kuwa katika mjengo huo.

Washiriki wenzake wamekuwa wakimtuhumu mshikaji huyo kunuka kikwapa na wengine kufikia hatua ya kumshitakia kwa Big Brother pale walipoitwa katika diary room.

Hata hiyo haijaweza kufahamika mara moja kama harufu hiyo mbaya inaokana na kutokuwa msafi ama ni ugonjwa kwani wapo wanaosumbuliwa na tatizo hilo hata kama watakuwa wakioga kila baada ya muda mfupi. Je, atatafutiwa dawa?Tuisubiri tuone.

Emma na Nkenna nusura watwangane!



Mshiriki wa Nigeria Nkenna na Mshiriki kutoka Angola nusura watwangane baada ya kufokeana wakiwa jikoni chanzo kikitajwa kuwa ni suala la usafi uliokuwa unatakiwa kufanyika katika chumba chao cha kulala.

Washiriki hao walionekana wakipandishiana na kufikia hatua ya kutaka kukunjana huku kila mmoja akimtolea mwenzake maneno machafu, hali iliyosababisha kukosekana kwa utulivu kwa sekunde kadhaa.

Hata hivyo, baadae mzuka wa wawili hao ulipungua na kuendelea kuwajibika kama kawaida.

Liz atoa ‘kitchen party’ kwa mabinti!



Mshiriki wa Afrika Kusini Liz wiki juzi kati alionekana akitoa ‘kitchen Party’ ya nguvu kwa washiriki wenzake wa kike pale alipokuwa amelala chumbani na kuwaeleza jinsi ya kufanya mapenzi wakiwa peke yao bila ya kumtegemea mwanaume.

Mwanadada huyo alikuwa akitoa somo hilo huku akionesha kwa vitendo akiwa amejikunyata kitandani, hali iliyowashangaza baadhi ya watazamaji ambao walishindwa kuamini kama binti hiyo angeweza kukosa aibu na kuongelea mambo hayo.

Katika kutoa maoni wapo waliomkejeli kwa kusema kuwa, anadhani kila mmoja anaweza kumuelewa kwa kitendo anachokifanya lakini mwenyewe akadai kwamba anachokifanya pale ni ‘game’ tu na si vinginevyo.

Eliza anamzimikia Kaone?


Wiki hii mwakilishi wetu katika shindano hilo, Elizabeth Gupta ameonekana kuwa karibu sana mshiriki kutoka Botswana KAone, hali inayowafanya watazamaji kujiuliza kama wawili hao wamezikinamna.

Eliza na Kaone juzi walionekana kutumia muda mwingi wakiwa wamejilaza kitandani huku wakizunguzmia masuala ya maisha lakini katika mazingira ua mtu na mpenzi wake.

Licha yakwamba hakuna kilihoendelea zaidi ya hilo lakini watabiri waneleza kuwa, ukaribu huo unaweza kuzaa uhusino wa kimalav huku wadau wakileza kuwa, hata Richard na Tatiana washiriki wa mwaka jana walioanza hivyo hivyo na baadae kujikuta wakizama katika dimbwi la mahaba.

Isabela akimbilia kwa Gaetana!


Wiki iliyopita katika tamthilia tumeona mengi ikiwa ni pamoja na Angela anakosa furaha pale anapokumbuka wimbo aliomchagulia baba yake.
Isabel anasafiri na kwenda Las Cruces, ambako atakutana moja kwa moja na Cantalicia.
Gaetana anamuota Cerinza akiumwa sana na anamuona vile anavyoteseka.
Antonio anagundua mambo ya ajabu yaliyomzunguka Salvador.
Abigail anapokea habari mbaya ya kifo cha mume wake na kwenda kutembelea kabuli lake.
nini kitatokea?Endelea kusoma…
Valeria anakiri kwa Simon kwamba siku zote anampenda Pedro José. Huku kwa akina
Isabel na Salvador baada ya kubaini ukweli kutoka kwa Cantalicia wanaamua kumsaidia kiasi Fulani cha pesa Cantalicia na Monchito.
Rebeca anakuwa hana muda wa kuandaa mkutano na Elizabeth na kuunda chuki kisha kujitetea kwa kutoa maoni kwa Salvador.
Kubwa kabisa, anasisitiza kwamba Isabela hatakiwi kuaminika kwasababu anashawishiwa kwamba kuna kitu anachokificha.
Isabel baada ya kuona mambo yamemuwia magumu anaamua kumtembelea Gaetana. Hata hivyo, mtabiri huyo anakuwa hayuko tayari kumpatia msaada na kukataa kisha akamuweka wazi na kumwambia kuwa inawezekana Peter Joseph na mume wake ambaye ni Salvador ni mtu mmoja.
Je Isabela atafanya nini baada ya kupewa live na Gaetana? Usikose uhondo wa tamthilia hii ambayo inaelekea ukingoni.

Wasanii wa filamu waicharukia BASATA!


Wadau pamoja na wasanii wa filamu nchini leo (Ijumaa) wanatarajia kukutana katika Uwanja wa Leaders Club ili kupinga uamuzi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kukataa kusajili chama chao kwa kile kilichodaiwa kuwa, nao walikuwa na lengo la kuanzisha chombo kama hicho.

Wasanii hao waliamua kuanzisha chama hicho walichokiita Tanzania Film Federation (TAFF) kwa lengo la kuwaunganisha na kutetea haki zao lakini BASATA waliwawekea ‘kauzibe’ hivyo kukubaliana kukutana ili kutafakari cha kufanya.

Wakiongea na Ijumaa juzi katika nyakati tofauti, wasanii hao walisema kuwa wamelishangaa sana Baraza hilo kwa kuwakwamisha katika jitihada zao za kutaka kuunda chombo cha kuwalea pamoja hivyo wameandaa mkutano huo ambao utawakutanisha wasanii wote nchini ili kuweka mikakati itakayowasaidia.

“Tumeandaa mkutano unaotarajia kufanyika siku ya Ijumaa (leo) kuanzia saa nane ili kuhakikisha tunapanga mikakati ya pamoja ili kuhakikisha tunakuwa kitu kimoja bila kuyumbishwa na watu wachache wanaotumia BASATA,” alisema Chekibudi.

Aidha, Ijumaa lilibahatika kuongea na mmoja wa maafisa wa BASATA aliyetambulika kwa jina la Omary Mayanga ambaye alikiri Baraza hilo kukataa kusajili chama hicho cha wasanii lakini kwa maelezo zaidi akamtaka mwandishi kuwasiliana na Katibu Mkuu.

TID, Banana waitosa Twanga!


Vinara wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini Khaleed Mohamed a.k.a TID na Banana Zahir Zorro waliwaacha watu hoi baada ya kugoma kupanda katika jukwaa la Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ ambayo ipo chini ya Kampuni ya ASET inayomilikiwa na Asha Baraka.

Tukio hilo lililopokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki, lilichukua nafasi wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo bendi hiyo hufanya vitu vyake kila Jumamosi.

TID na Banana walionekana kuwepo ukumbini humo wakifuatilia kwa makini onesho hilo huku mara nyingi wanamuziki wa bendi hiyo wakiwarusha kama ishara ya kutambua uwepo wao.

Hata hivyo baadaye, wanamuziki wa bendi mbalimbali walipotakiwa kupanda jukwaani kwa ajili ya kuwasalimia mashabiki, wasanii hao hawakuonekana!

“Naam, wasanii huwa tunasalimiana kisanii, hivyo nawaomba wasanii wote ambao mpo humu ndani, mje kuwasalimia mashabiki....” Charles Gabriel a.k.a Charles Baba alisikika akisema.

Wasanii wengine wakiwemo Badi Bakule na Jua Kali wa Tanzania One Theather ‘T Respect’ walipanda jukwaani na kukonga nyoyo za mashabiki, lakini mastaa hao wa Bongo Fleva hawakutia timu.

“Wapi Banana na TID, tunawasubiri mbele jamani, njoeni...njoeni jamani...” Charles Baba alizidi kuwaomba wapande lakini hawakutokea.

Baada ya kuitwa kwa muda mrefu na kuonekana kutokuwa na mpango wa kupanda jukaani, Badi Bakule na Jua Kali kwa nyakati tofauti waliwasha moto ambapo waliwakuna sana mashabiki.

RAY C MBARONI



Msanii wa kike anayesumbua katika muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila a.k.a Ray C hivi karibuni alijikuta akitiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa madai ya kumtapeli promota wake aliyetambulika kwa jina la David Masatu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Ray C alinaswa mwishoni mwa wiki iliyopita na ‘Vijana wa Mwema’ wa kituo hicho akidaiwa kutia ndani kiasi cha shilingi 600,000 za promota huyo alizopewa ili ikafanye shoo mkoani Mwanza.


Ilidaiwa kuwa, baada ya mwanadada huyo kupewa mkwanja huo kama ‘advansi’ kufuatia makubaliano ya kufanya shoo mbili kwa shilingi 1,200,000, siku ya kukwea pia kuelekea Rock City ilipowadia, alikuwa hapatikani hewani.

Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya promotoa huyo kubaini kuwa kaingizwa mjini alikwenda katika kituo cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia Ray C kesi yenye jalada namba OB/RB/17123/09, KUTAPELI.

Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita (Jumapili) msanii huyo alinaswa na polisi kisha kufikishwa katika kituo hicho na kuhojiwa kwa saa kadhaa.

Baada ya kufikishwa kituoni hapo, msanii huyo aliomba ishu isiende mbali na kuahidi kurudisha nusu ya pesa alizopewa (300,000) huku akiomba apewe siku 14 kutekeleza hilo ambapo alikubaliwa kisha kujidhamini mwenyewe.

Saturday, September 19, 2009

The longest fingernails on both hands..


Nelvin feyzel booz from the city of pontisc,Michigan not strig nails25 yrs,bringing the total length of 1910 amounted to 931 nails see.

The largest number of needles in the head.


One 1,790 needles for acupuncture was votknuto in the head and face Shengchu Chinese Wei (Wei Shengchu) on March 23, 2004 in the city of Nanning, China.

Hii ni hatari


Harry Turner (Garry Turner) from Britain could spread to the abdominal skin to see 15,8 This is due to a rare disease known as syndrome Elersa- Danlosa violation connective tissue, affecting the skin, ligaments and internal organs. Collagen, strengthens skin, and is responsible for its elasticity, damaged, which, among other things, is the weakening of the skin and joints razboltannost. In more severe cases, this can result in the destruction or rupture of blood vessels, leading to death.

The largest number of snakes gremuchih held in his mouth.


American Jackie Bibby (Jackie Bibby) was able to hold in his mouth without assistance 10 gremuchih snake tails for a period of 10 seconds on the Day Guinness World Records on November 9, 2006

God gives us a lot of graces






God has given us a lot of graces, but we forget all. The small child gives us a lot to think of us.

Friday, September 18, 2009

Thursday, September 17, 2009

mambo ya massage


massage si kwa wanadamu tu hata wanyama nao wamo.

Natural shampoo


Kwanini uangaike kwenda saruni madukani wakati unangombe wako nyumbani anatoa vitu natural

Kiboko si mchezo


Waliokataza wanafunzi kupigwa viboko waliona mbali,sasa ona huyu makalio yameyeyuka kwa kuchapwa bakola.

Teamwork mwana


Baada ya kuzidiwa na njaa wanaamua kusaidiana kutafuta chakula

Mungu na maajabu yake


huyu ana sikio mkononi,haijawahi tokea

Si kwenye siasa tu


Mzee Obama hata kwenye michezo yumo,nzuri zaidi First lady ahachwi nyuma

Aamua kujiajiri mwenyewe


Kazi bwana si mpaka utafutiwe eneo la kufanyia,kuliko kuiba bora utafute ubaraza na kidressing table cha aina mambo yanakwenda unajipatia ulaji.Yanini uchomwe moto.

Tuesday, September 15, 2009

Huu ndio mwisho wa wapendanao Amina na mpakanjia





ENZI ZA MAISHA YA
UPENDO YA AMINA NA
MEDDY MPAKANJIA

Maisha ya
m a r e h e m u
A m i n a
Chifupa na
M o h a m e d
Mkapanjia a.k.a Meddy
yalikuwa ya upendo
wa dhati ndiyo maana
watu wengi walikuwa
wakiyatafsiri kuwa ni ya
kutegemeana. Kupendana
kwao huko kumezua
minong’ono kwa watu
mbalimbali wakidai huenda
mkewe amemchukua.
Hata hivyo, inabaki kuwa
kazi ya Mungu haina
makosa.
Historia yao kwa ufupi:
Amina alizaliwa 1981-2007
alikufa akiwa na miaka (26)
Meddy alizaliwa mwaka
1972-2009 amekufa akiwa
na miaka (37)
Historia ya ndoa yao:
Walioana mwaka 2001
Amina akiwa ni mjamzito
wa miezi saba.
Walijaaliwa kupata mtoto
wao wa kwanza Rahman
‘Ramanino’ mwaka 2002.
Baada ya hapo mapenzi
yao yalikuwa motomoto
walikuwa wanandoa
waliofuatana kila kona hasa
kwenye kumbi za starehe.
Amina alikuwa ni
mshereheshaji wa shughuli
‘MC’ na pale alipokuwa
akiwajibika mume wake
alikuwa pembeni yake,
hakika walipendana na
ndiyo maana baada ya kifo
cha Amina Chifupa afya ya
Mpakanjia ilianza kuwa tete
kwani alianza kuandamwa
na msongo wa mawazo na
maradhi kadhaa kutokana
na upweke wa kuondokewa
na kipenzi chake.
Amina na Mpakanjia wote
walifia katika Hospitali
ya Jeshi ya Lugalo baada
ya kulazwa kwa muda
mchache huku Meddy
akidaiwa kufa kwa Homa
ya matumbo ‘Typhoid’
na Amina arifariki kwa
matatizo ya msongo wa
mawazo.
Mwisho naweza kusema
kuwa maisha yao yalikuwa
ya upendo na wamemuacha
mtoto wao Rahmanino
katika hali ya uzuni. Mungu
awalaze pema peponi.
Amini.
***
MEDDY MPAKANJIA:
ILIKUWA LAZIMA AFE
Mohamed Mpakanjia
a.k.a Meddy Mpakanjia,
inaonekana ilikuwa lazima
afe kutokana na ‘midomo’
ya watu ambapo tangu kifo
cha mkewe, Amina wamekuwa wakisema
hata yeye asingeishi sana.
Mbali na uchuro huo, taarifa za uvumi
wa kifo chake zilizokuwa zikienezwa kwa
njia ya mitandao na vyombo vya habari,
ilikuwa ikitikisa uhai wake kwa muda
mrefu.
Kwa mara ya kwanza, Mpakanjia
alizushiwa kifo mwezi Agosti mwaka
2007 baada ya kuugua na kulazwa katika
Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) Lugalo, kisha vyombo
vya habari vikaripoti kuwa alikuwa
ameaga dunia.
Tangu kipindi hicho, Mpakanjia alikuwa
akidai kushindwa kuzuia hisia zake za
kumpenda mkewe aliyemuacha wakiwa
bado wana pendo la dhati na kusababisha
kuzibandua picha zote za Amina
zilizokuwa ukutani mwa nyumba yake
kwa lengo la kupoteza kumbukumbu.
Wachunguzi wa masuala ya saikolojia
walisema kuwa, Mpakanjia aliathirika
kisaikoloji na kujikuta anakuwa na
msongo wa mawazo kutokana na kuishi
akiwa mpweke. Aidha, wataalam wa
maisha wanadai kuwa, mara nyingi mke
akitangulia kufa, mume naye haishi miaka mingi

Saturday, September 12, 2009

Mimi na mwanangu mzuri tunapendana hao



My baby Jorii, au mzuri upendavyo wewe kumuita.
I love her so much.
namuomba mungu anikuzie...

Friday, September 11, 2009

Mwana hufuata nyayo za wazazi!




Mambo haya bwana huanzia utotoni, unaweza kukaa ukajiuliza hivi mwanangu mtundu kumbe kile unachofanya mzazi naye anajifunza toka mdogo, kwa wenzetu wazungu hapa ndio mwanya wa kumjua mtoto ana kipaji gani na kumfatilia kwa karibu kwa sisi watanzania hatuna muda na watoto wetu kwa baadhi ya wazazi..ndio maana mwisho wao wengine huishia pabaya lakini endapo mtoto utajua ana kipaji gani na kumuendeleza aisee utashangaa..
wazazi jaribuni kukaa na watoto mtajua tu na kuwajengea maisha bora kwa kufata hisia na muelekeo wao tokea uchanga wao.

Gaga na ujio mpya wa miwani




Huyu ni Lady Gaga supastaa anayeogoza kwa kuvaa vichupi..
Hapa anaonekana katika sura mpya baada ya kubadiri miwani.Hii ni kwasababu miwani yake iliyokuwa ikimpatia umaarufu kuibiwa katika shoo moja aliyoenda kufanya huko London mapema mwaka huu.

EXCLUSIVE: Edna katika harakati za kuendesha mkoko


Mtoto alipotua nchi Fulani kuchukua mkoko wake, si mchezo alianza kwa kuendesha bajaji Huyu taratibu kavuta mkoko wa kikubwa.. kifupi namheshimu sijui mimi ntaanza na nini wakati hata mkokoteni mbinde kazii hiyooo ujue...

Halle Berry mvuto mpaka ujauzitoni


Hapa akitoka kwenda Clinic kwakeli anatamanisha..


Wengine wakibeba shepu huyeyuka yeye ndo kwanza kijungu kinafumuka...

Hii ni kufuru





Jamani hii si ni kufuru kwa watanzania ukifanya pati hii kabla hujapata mtoto wenye imani zao husema ya kwao lakini kwa wenzetu ni vitu vya kawaida na mungu huwanyooshea maisha na kuwa kama yalivyopangwa.
Hapa mwanadada Kendra ameandaliwa pati wenyewe wanaiita 'Baby Shower paty' hii ni pati kabla ya kujifungua ambayo waliyoilenga ni kukusanya vitu vya mtoto bila kuacha hata nukta kwa maana hiyo ni mazagazaga kibao...
Tanzania huenda ikaingia hii, je wataichukulia vip? mimi na wewe hatujui lakini wengi utasikia si kufuru hii wenye imani zao sasa..
mimi nimeipenda hiyo huenda nikamfanyia Roby Chacha ambaye anatarajia kupata kibebi siku za usoni..Nakuombea rafiki yangu ujifungue salama.