Miaka ikapita akiwa huko mtaani, siku moja akavamiwa na mlevi. Baada ya hapo akawa anapata ndoto mbaya na kujikuta akiwachukia wanaume.
Candelaria, mwanamke mmoja ambaye kazi yake ni Udobi anampa ofa ya kukaa nyumbani kwake na kumchukulia Marichury
Siku moja, Marichuy anasababisha fujo na kupelekwa mahakamani ambapo anakwenda kukutana na Jaji ambaye ni baba yake wa Damu, (Ingawa hakuna kati
Kwa upande mwingine Juan Miguel San Roman, ambaye alifanikiwa kuokoka katika ajali ya ndege , hakuwa akimpenda mke wake Viviana, anaamini kuwa Marichuy ni msichana asiyekuwa na tatizo.
Hata hivyo Viviana anakuwa mzima anaamua kuishi maisha ya starehe bila kuifahamisha familia yake kuwa yuko hai.
Marichuy anasaidiwa na mwanasaikolojia ambaye ni Juan Miguel San Roman, ambaye anataka kuona mazuri kwa Marichuy.
Marichuy anaachiwa huru kwa dhamana ya Juan Miguel na akapanga mpango wa kuishi naye nyumbani kwake pamoja na mtoto wake, Mayita, mama mkwe wake, Onelia, na dada yake ,Rosio.
Wakati Marichuy akiwa kwenye nyumba ya Migel wakajikuta wamekuwa wapenzi. Lakini Juan Miguel anaamua kumpeleka Marichuy kwenye nyumba ya Velarde ili kulikuza penzi lao.
Estefania yeye anamchukia Marichuy kwasababu yeye pia anampenda Juan Miguel. Estefania na shangazi yake, Isabella, wanagundua kuwa Marichuy ni mtoto wa Velardes, wanamfanyia mbaya Marichuy na kumfanya aonekane mwizi ambaye alimuibia Velardes.
Cecilia anawaonya Estefania na Marichuy. Hata hivyo Estefania anafanikiwa kuanzisha uhusiano na Juan Miguel, kitendo kinachomtia wivu Marichuy.
Baada ya Patricio kuupata uongo wa Marichuy na tabia zake, Marichuy anaamua kumwambia Juan Miguel kwamba anataka kuishi na yeye, kwasababu hataki kukaa na Velardes.
Juan Miguel anakubari maombi ya Marichuy na kumchukua wakaishi pamoja.. je watu hawa watakuwa mke na mume?
Juan Miguel anagundua kuwa yeye ndio alimvamia Marichuy alipokuwa mdogo lakini Marichuy anashindwa kutambua ni jinsi gani ilitokea. Pale Juan Miguel alipoanza kumuepuka akihisi makosa yake na huenda Marichuy akamgundua, Marichury akaanza kudhani huenda Juan Miguel anamchukia, ambapo alimua kuwambia kuwa anampenda.
Juan Miguel anapanga mpango wa kumuoa.. Lakini anashindwa atafanyaje kwani tatizo ni lile alilowahi kufamfanyia alipokuwa mdogo.
Padre Anselmo na Eduardo (rafiki wa kuaminika wa Juan Miguel ) wanamuonya Juan Miguel amwambie kumwambia marichuy kabla hajamuoa kuwa yeye ndio aliyemvamia wakati akiwa mtoto lakini Miguel akahofia huenda akaharibu mapenzi
Wakaamua kufunga ndoa na kwenda kwenye fungate la maana.
Asubuhi Marichuy anapoamka anaamkia kwenye ndoto akiwa amegundua kuwa mbakaji wake ni Juan Miguel.
Miguel akamuomba msamaha kwa kitendo kile lakini hakukubari kutoa msamaha na kuamua kurudi kuishi na Candelaria.
Siku chache baada ya tukio, Juan Miguel anatembelea chama kimoja na huko anagundua mgonjwa mwingine. Kwa wasiwasi mkumbwa, akamuona mke wake ambaye alitakiwa kuwa mfu. Kwa wakati huo,akachukua jukumu la kujua kilichotokea kwa mkewe na kumsaidia kurudi katika hali yake ya kawaida.
Je itakuwaje kwa Marichuy atamsamehe Miguel au atamrudua mke wake…Hii ni
Intro ya Tamthilia muendelezo kamili Utaanza wiki ijayo…
No comments:
Post a Comment