.
Wednesday, May 19, 2010
Harufu zinazosaidia kuwa na kumbukumbu, nguvu na mood nzuri ni kama zifuatazo:
Harufu za matunda ya aina mbalimbali yapatayo tisa husaidia kuimarisha afya yako ikiwa ni pamoja na kukufanya ujisikie vizuri, leo nitaongelea harufu tatu kwa kuanzia ambazo ni tiba tosha kwa hayo niliyoyataja hapo juu
Harufu ya Tofaa la kijani ‘Green Apple’
Harufu ya tunda hili inaweza kukusaidia kupata hisia za kimapenzi na kukuweka katika hali ya furaha wakati wote, harufu hii imethibitishwa na Alan Hirsch, mkurugenzi wa utafiti wa harufu na ladha wa huko Chicago.
Mtafiti huyo anayataja matunda mengine kuwa ni banana, na piripiri manga.
***
Vuta harufu: ya chenza au Mrujuani
Kwa wenzetu waaustria, wamejifunza kuvuta harufu ya chenza kabla ya kufanya chochote na vile vile mrujuani kabla ya kufanya chochote..
Harufu hizi huwasaidia kuondoa wasiwasi pamoja kuwatuliza kama wako katika hali mbaya ya mwili kama woga na kutojisikia huru.
Jaribu kufanya hivi: Chukua kiasi kidogo cha tone la mafuta ya mrujuani paka usoni na pakaa wakati unaenda kazini kwa wale wanaofanya kazi itaondoa ‘stress’ zote na utaishi kwa amani.
Wiki ijayo nitaelezea harufu nyingine nzuri zinazoweza kuimarisha afya yako.
Harufu nyingine nzuri ni Chokolate, hii husaidia kuleta hisia za mapenzi, jamani vitu hivi watu wanavidharau lakini vina ukweli emu jaribuni muone... ni taaaaaaaaamu. harufu sasa usiseme inasisimua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment