.
Saturday, August 22, 2009
WANAMUZIKI WA HIP HOP WENYE FEDHA NYINGI DUNIA
Hakuna asiyeelewa kuwa sanaa ya muziki wowote
ukitumika vema ni ajira tosha kwa wahusika ambao
mara nyingi mkwanja wanaoupata ni mkubwa kuliko
mtu aliyeajiriwa.
Ili kudhibitisha kile ninachokisema, leo nimelazimika
kuwamulika wanamuziki wa muziki 20 wa Hip hop
nchini Marekani ambao wanaishi maisha ya kifahari
kutokana na kazi yao hiyo.
Mwanamuziki anayewaburuza wenzake kwa kuwa
na fedha nyingi ‘The Big Boss’ ni Shawn Carter a.k.a
Jay-Z ambaye anamiliki Dola za kimarekani milioni 34.
Jamaa huyo aliyetangaza kuachana na masuala ya muziki
mwaka 2003, amerudi kwa kasi kubwa katika ‘game’ na
kibao chake cha ‘Last year’s Kingdom Come’, ambacho
kiliingia katika chati za Billboard za Pop na Rap. Pamoja
na muziki, Jay-Z ni ‘big bosi’ wa Studio za Def Jam,
zilizopo Brooklyn nchini humo.
‘Jiga’ anamiliki asilimia 40 ya mikataba ya nyumba za
starehe na ‘shea’ zake za hisa. Hivi karibuni ziliibuka
habari kuwa, Jay-Z ataondoka kwenye kampuni hiyo
na kujiunga na mpenzi wake, Beyonce Knowles katika
Kampuni ya ‘Colombia Records’ kwa lengo la kujipatia
pesa nyingi zaidi.
***
Curtis Jackson a.k.a 50 Cent anashika nafasi ya pili kwa
kumiliki kiasi cha dola za kimarekani milioni 32.
50 Cent ambaye kwa sasa ni msimamizi wa Kundi la
G-Unit, akiwa anashikilia sehemu kubwa ya burudani
kwa kusimamia Lebo za wanamuziki (Lloyd Banks, Mobb
Deep), ambao wamekuwa wakitokea kwenye milio ya
simu, michezo
ya video na
sherehe za mitaani.
Mwaka 2004, alikubali kuzuia maji ya Vitamini kwa
kubadilishana ‘shea’ ndogo, ambapo mwaka huo huo
mwezi Mei, Coca-Cola walisema kuwa watanunua maji
ya vitamini ‘Vitamin Water’ kwa dola za kimarekani
bilioni 4.2.
50 alifanikiwa kuchukua kwa dola milioni 100. Mwaka
2003, alifanikiwa kununua nyumba kwa kiasi cha dola za
kimarekani milioni 4, ambayo tayari ametangaza kuiuza
kwa dola milioni 20. 50 anatarajia kutoa albamu yake ya
tatu Septemba mwaka huu.
***
Mtu mzima Sean Combs a.k.a Puff Daddy a.k.a P.
Diddy, anakamata nafasi ya tatu kati ya wanamuziki
ishirini wanaodaiwa kuwa na pesa nyingi akimiliki Dola
za kimarekani milioni 28.
Ni vibao viwili vya ‘Bad Boy’ na ‘Warner-backed’ kabla
ya ‘I need a girl’ vilivyomuingizia burungutu la noti
ambapo mwaka jana alitoa albamu moja akishirikiana na
Danity Kane, Cassie na Yung Joc. Mwaka huo huo, Diddy
alitoa albamu yake aliyoiita Press Play, albamu yake ya
kwanza ambayo aliitoa kwa muda wa miaka minne tangu
aingie kwenye game, aliingiza pesa nyingi zilizojalizwa
na lebo za nguo bila kutarajia kutoka kwa Sean John.
***
NO. 4
Timothy Mosley a.k.a Timbaland ni mwanamuziki
mwingine ambaye anashikilia nafasi ya nne ya
wanamuziki wa Pop wenye pesa, yeye anashikilia dola
milioni 21.
Mwanamuziki huyu ambaye amevuma kwa muziki wa
Pop na Hip-hop ameweza kujipatia pesa nyingi kupitia
albamu yake kubwa aliyoitoa mwaka jana akimshirikisha
Nelly Furtado iliyokwenda kwa jina la ‘Loose’ ile ya
kwake inayoitwa FutureSex/
LoveSounds.
Mwaka 2006, Timberland aliandaa nyimbo zake na
kufanikiwa kuingia katika ‘chati’ kubwa kubwa ya
nyimbo huko marekani.
***
NO. 5
Andre Young a.k.a Dr. Dre, naye ni mwanamuziki
ambaye anashikilia namba tano akimiliki dola milion 20
za Kimarecani.
Ni mmoja wa waanzilishi wa Kundi la Rap la NWA,
ambaye amekuwa akifanya kazi katika albamu za
mjumuiko za wasanii wenzake kama Snoop Dog na
Eminem kwenye albamu ya ‘The Slim Shady LP’.
Amekuwa akiendesha burudani kila mwezi, akitumia
lebo mbalimbali zilizovuma na zinazovuma. Mwaka
jana aliandaa nyimbo ya Nas Escober na Jay-Z, ikiwa ni
pamoja na nyimbo nyingine nyingi katika ‘masongi’ ya
washkaji hao.
Ingawa imechukua miaka saba tangu alipotoa albamu
yake, ‘Dre’s classics baada ya lile songi la ‘The Chronic’
ambao bado anauza mpaka sasa na amefanikiwa kuuza
baadhi ya kopi zipatazo 250,000 kwa mwaka jana.
***
NO. 6
Marshall Mothers a.k.a Eminem a.k.a Slim Shady yeye
tayari kibindoni ana dola za kimarekami milioni 18.
Mwana-hiphop huyu ingawa anasema kuwa anaingiliwa
katika biashara ya muziki wake.
Eminem alifanikiwa kuuza ‘kopi’ lukuki za
albamu yake na kujiingizia kitita cha mihela kwenye
wimbo huo alioshirikiana na Akon uliotambulika kwa
jina la ‘Smack That’
***
NO. 7
Calvin Broadus a.k.a Snoop Doggy
Zao lingine la Hip hop ambalo linashikilia mkwanja
mnene wa dola za kimarekani milioni 17.
Snoop ni mwanamuziki mwenye jina katika
albamu ya Dr. Dre ya landmark, na The
Chronic ya mwaka 1992, kisha akafanikiwa kutoka
kivyake na kitu chake alichokiita Doggy style ambacho
kilimfanikisha kuingia katika ‘chati’ za juu za Billboard.
Mwaka jana Novemba kwenye tuzo za ‘Grammy’
walifanikiwa kuingiza albamu nane za kila mwanamuziki
huku singo ya Snoop iliyoitwa Doggystyle ikifanikiwa
kuingizwa kwenye moja ya albamu ambayo ilifanikiwa
kumuingizia pesa nyingi.
***
No. 8
Kanye West : Rapa mwingine aliyeshika namba nane
kwa utajiri ambaye amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dola
za kimarekani milioni 17.
Mbali na kufoka, Kanye ni muandaaji wa muziki
ambaye alifanikiwa kupata tuzo za Grammy, uandaaji
bora na uimbaji wa muziki wa kufoka.
Novemba mwaka jana alifanikiwa kuondoka na
tuzo ya MTV Europe Awards baada ya kuwa na video
bora ambayo ndio ilimuingiza katika shindano hilo na
kufanikiwa kushinda.
Muandaaji huyo amekuwa akijitafutia pesa kwa kuandaa
nyimbo za wasanii wenzake pamoja na kuwa muimbaji
ameweza kuadaa nyimbo moja ya mwanamuziki John
Legend, Jay-Z na Nas ambaye alivuma nayo mwaka
jana.
***
NO. 9
Pharrell Williams: Ni miongoni mwa
wanamuziki wanaomiliki mamilio ya dola ambaye tayari
ametia kibindoni dola za kimarekani zipatazo milioni
17.
Mwanahip hop huyu ana mafanikio madogo lakini
pamoja na mafanikio hayo ameweza kumiliki pesa
nyingi na hatimaye kuingia katika mpambano na kushika
namba tisa huku akijipatia heshima kubwa.
Ni mwanamuziki aliyeunda Timu ya ‘The Neptune’
ambaye ameweza kufanikiwa kutokana na kazi zake
za kuweza kuweka milio ‘beats’ katika nyimbo za
wanamuziki maarufu kama vile Jay-Z, Snoop Doggy na
Justin Timberlake.
Mbali na uimbaji mwanamuziki huyu amekuwa ni
mwa n ami t i n d o
ambaye hapitwi na wakati katika mavazi.
***
NO. 10
Scott Storc: Naye amekuwa miongoni mwa wanamuziki
ambao wanakimbiza kwa mapesa huku akiwa na kiasi
cha dola za kimarekani milioni 17. Yeye ameshika namba
10 kati ya watu ishirini.
Mwanamuziki huyu amejizolea mapesa kutokana na
matayarisho ya nyimbo za wanamuziki 50 Cent (Candy
Shop), Beyonce (Naughty Boy), Justin Timberlake (Cry
Me a River), na nyingine kibao.
Ada ya nyimbo ambazo amekuwa akiandaa ni dola
za kimarekani 85,000 kwa nyimbo moja. Mwaka jana
alifanikiwa kuandaa nyimbo 75, ukiwemo wimbo wa
Paris Hilton (Stars are Blind). Akiwa anafanya kazi chini
ya label yake amesema kuwa safari hii anatarajia kufanya
kazi na Paris Hilton kwenye Albamu yake.
***
Wengine waliofuata ni pamoja na Christopher Bridges
a.k.a Ludacris yeye anamiliki dola za kimarekani milioni
16, huku aliyeshika namba 12, Clifford Harris a.k.a T.I
akiwa anamiliki dola za kimarekani milioni 16.
Wengine ni Patton na Andre, hawa wanajiita Outcast
ambao wanamiliki dola milioni 14, wakiwa kama kundi
moja la Hip hop, wao wameshika namba 13 wakifungana
na Jonathan Smith a.k.a Lil Jon anayemiliki dola za
kimarekani milioni 14, akifuatiwa na O’Shea Jackson
a.k.a Ice Cube mwenye kitita cha dola za kimarekani
milioni 13 akishika namba 15.
Wanahiphop watano waliobaki wenye pesa ili kufi kia
ishirini ni pamoja na Germaine Dupre anayeshikilia
namba 16 akimiliki kitita cha dola za kimarekani
milioni 12 akifuatiwa na Kasseem Dean ‘Swizz Beatz’
yeye anahifadhi dola za Kimarekani milioni 12 akiwa
amesimamia kwenye namba 17.
Aliyeshika namba 18 ni Hakeem Seriki ‘Chamillionaire’,
yeye anamiliki dola za kimarekani milioni 11 akifungana
na Jayceon Taylor ‘The Game’ mwenye kitita cha dola za
kimarekani milioni 11 aliyeshika namba 19.
Aliyefunga mkia katika ishirini bora ni Jasiel Robinson
‘Yung Joc,’ yeye anamiliki kitita cha Dola za kimarekani
milioni 10
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment