Imeelezwa kuwa, mwanamuziki wa POP nchini
Marekani, Britney Spears, amepingwa kibuti
(ameachwa) na mpenzi wake aliyejulikana kwa
jina la Jason Trawick baada ya kulazimisha
ndoa.
Habari kutoka kwenye mtandao zinadai kuwa,
penzi la wapendanao hao lilidumu kwa muda
wa miezi mitano, ndipo mrembo akaonekana
kukolea na kumlazimisha jamaa amchukue
jumla jumla badala ya kukutana kwa msimu,
lakini mwenzake alikuwa hana nia hiyo na kuamua kuvunja
mahusiano yao.
Rafi ki wa karibu wa wapenzi hao ambaye hakupenda
kutaja jina lake, aliliambia jarida la National Enquirer kuwa,
binafsi alitambua mapema kama penzi lao halitadumu
kutokana na Trawick kutoonyesha dalili zozote za kufunga
pingu za maisha licha ya kumvalisha pete ya uchumba
ambayo nayo alimvisha kwa shingo upande.
“ Mara kwa mara nilimwambia Britney kuwa, Trawick
hatamuoa kutokana na kupenda vimwana wengine bila
kujali uchumba wao, lakini mwanadada huyo hakuniamini,
baada ya kuwa na matumaini kwamba siku moja angeacha
tabia hiyo na kuoana.” alisema swahiba huyo.
Aliendelea kusasambua kuwa, juhudi za Britney
kumshawishi Trawick amuoe lionekana kuingia nyongo
baada ya kuambiwa kwamba jamaa bado anahitaji muda
wa kujirusha na vimwana wengine kabla ya kuingia katika
kitanzi cha ndoa.
Kauli hiyo ilimvunja moyo Britney na kujiona kama hana
bahati ya kuolewa maishani mwake, baada ya kuachika
mara mbili.
Amewahi kuolewa mara mbili kabla ya kukutana na
Jason Trawick. Kwa mara ya kwanza aliolewa na Jason
Alexander, akaachika, akachukuliwa na Kevin Federline
na kufanikiwa kupata watoto wawili Sean Preston, (3),
na Jayden James (2) kabla ya kutoswa kisha kumganda
Trawick ili awe wake wa maisha.
Hivi karibuni, Britney alionekana Los Angeles Hotel
akijiachia kwenye bwawa la kuogelea ambako alishinda
siku nzima akiwa amevaa bikini yake ya pink
ambayo ilimpendeza sana huku akionekana
kujifariji kivyake baada kutoswa.
HISTORIA YAKE KWA UFUPI!
Britney Spears alizaliwa
Desemba 2, 1981 huko
Mississippi na kukulia
Louisiana. Ni mwanamuziki
wa Marekani na alianza
kuonekana kwenye runinga
nchini humo mwaka 1992
kama mshiriki wa program
ya Star Search. Baada ya
hapo, alijiunga na kipindi
cha televisheni cha The New
Mickey Mouse Club mwaka
1993 mpaka 1994.
Mwaka 1997, Spears alisaini
mkataba wa kurekodi na Jive,
na kufanikiwa kutoa albamu
yake aliyoiita Baby One More
Time ambayo ilitoka mwaka
1999.
Albamu hiyo ilifanikiwa kuingia
kwenye chati 200 za Billboard.
No comments:
Post a Comment