.
Saturday, August 22, 2009
Tiger Woods
mwanamichezo
tajiri kuliko wote
duniani !
Mtoto Sam akipokezwa
kwa baba yake
Tyra Banks aliyewahi
kutoka na Tiger Wood
Tiger Wood akiwa na
mkewe
Tiger akiwa na Rais
Obama
Tiger akiwa na familia
yake mke na watoto
Tiger Wood akiwa na
mke wake
ANAYEWACHUKIA MAPAPARAZZI.
Habari zake binafsi:
Alizaliwa kwa jina la Eldrick Tont
Woods
JINA LAKE LA UTANI NI TIGER
Alizaliwa December 30, 1975 huko Cypress,
California.
Ana urefu wa futi 6 na uzito wake ni kilo
84.
Kwa sasa tajiri huyu anaishi Windermere,
Florida
Mke wake ni Elin Nordegren (alimuoa
mwaka 2004)
Ana watoto wawili wanaitwa Sam Alexis
(aliyezaliwa 2007)
Na Charlie Axel ambaye amezaliwa mwaka
huu (2009)
ELIMU
Tiger Woods alisoma Stanford University.Aliingia rasmi kwenye mchezo wa golfu
mwaka 1996
Michuano aliyowahi kushiriki na kushinda
Mpaka mwaka huu ameshashinda michezo
92 ya Golfu
Kwa michuano ya PGA ameshashinda
michezo 68 ( mara tatu wakati wote)
Michuano ya ulaya ameshinda mara 36
Michuano ya Japan mara 2
Michuano ya Asian mara 1
Michezo mingine ameshinda mara 14
Baadhi ya Zawadi alizowahi kupata za ushindi
katika mchezo wake wa golfu ni
Mshindi wa Manchester (The Manchester
winner ) miaka ya : 1997, 2001, 2002, 2005
U.S. Open miaka ya 2000, 2002, 2008
Open Championship miaka ya : 2000, 2005,
2006
PGA Championship miaka ya : 1999, 2000,
2006, 2007
MASLAHI ALIYOWAHI KUINGIZA
Ni mwanamichezo ambaye aliingiza pesa
nyingi mwaka 2008 kwa kukadiriwa kuwa
na kiasi cha dola million 110 na kufanikiwa
kuungwa mkono na mashabiki wa mchezo wa
Golfu .
MAISHA YAKE YA NDOA
October 5, 2004. alifunga pingu za maisha
na mwanamitindo mzaliwa wa Sweden Elin
Nordegren, ambaye alimposa akiwa na umri wa
miaka 27 huku Elin akiwa na miaka 23.
WAPI WALIKUTANA
Elin na Tiger walikutana mwaka 2001 huko
England. Elin alikuwa akifanya kazi kwa Jesper
Parnevik, mcheza golfu ambaye ni mzaliwa wa
Sweden.
ANAWAZINGUMZIAJE MAPAPARAZZI:
Ni mwanamichezo ambaye hapendi sana
kuandikwa na kutangazwa kwenye magazeti
hasa habari zake za ndani.
Anadai kuwa haoni sababu ya mambo yake
ya siri kuwa yakianikwa lakini kwa sababu
ni staa na mara nyingi umbea ‘gossips’ ndio
unauza hana njia anatakiwa kukubaliana
nao.
Amewaongelea mapaparazi kwa njia
nyingine ambayo inamuonesha kukerwa
nao kwa kusema kuwa “Sikuona sababu
ya wao kuingilia harusi yangu na kupiga
picha lukuki lakini kwa sababu ni wambea na
umbea unapendwa sikuwa na njia” alisema
alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi
wa kujitegemea Melisa Stark.
WANAWAKE AMBAO AMEWAHI
KUTOKA NAO.
Amewahi kujichanganya na Brooke Langton,
Gabrielle Reece
Tyce Nahles, Tyra Banks, Joanna Jones,
Kasmira Karanji na wa mwisho ni mkewe Elin
Nordergen ambaye yuko naye mpaka sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment