.
Monday, August 31, 2009
Heidi na mumewe wafanya mapenzi hadharani!
Mwanamuziki wa miondoko
ya Pop, ambaye pia ni
mtangazaji wa runinga
moja nchini Marekani Heid
Montag, amewashangaza
watu wengi waliokuwa wamejipumzisha
kwenye ufukwe wa Bahamas nchini humo
baada ya kufanya mapenzi hadharani
bila kujali umati wa watu uliokuwa
unawaangalia.
Habari zilizosambazwa kwenye mtandao
mmoja zinasema kuwa, Heid akiwa na
mumewe mpya aliyetajwa kwa jina la
Spencer Pratt, walikwenda katika ufukwe
huo kujipongeza baada ya mwanadada
huyo kufanikiwa kutumbuiza vema katika
shindano la kumtafuta Miss Universe
lililofanyika mwisho mwa wiki iliyopita.
Wapendanao hao, baada ya kufanya
mambo ya chumbani ‘live’ walianza
kuongelea huku wakikimbizana kama
watoto wadogo, hali iliyowafanya
waonekane kama vituko.
Wapenzi hao hawakuona ajabu kupigwa
picha pamoja na vijembe walivyokuwa
wanatupiwa na walioshuhudia tukio hilo.
Kwa kifupi:
Heid Montag, anafahamika kama ‘Heidi
Pratt’
Alizaliwa September 15, 1986
Umri wake ni miaka 22
Mzaliwa wa Los Angeles, California
Anaimba muziki wa Pop
Kazi yake ni mtangazaji wa Television ,
mwanamuziki na muandishi wa nyimbo
Pia ni muingizaji wa sauti katika
nyimbo.
Mwaka alioanza kusikika ni mwaka
2005
Anafahamika zaidi katika Label ya
Warner Bros. na Heidi Pratt
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment