.
Saturday, August 22, 2009
JENNIFER LOPEZ
JENNIFER LOPEZ
Hivi karibuni Jennifer
Lopez alisheherekea
miaka arobaini ya
kuzaliwa kwake
na kupongezwa na
mashabiki na marafi ki
zake waliohudhuria
hafl a fupi ambayo iliandaliwa na mumewe,
Marc Anthony.
Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi
uliofahamika kwa jina la The Edison
Ballroom uliopo Jiji la New York.
Maswahiba zake Ricky Martin, Liza
Minnelli na muandaaji wa muziki,
Benny Medina ni miongoni mwa watu
walionogesha shughuli hiyo ambayo
hufanyika mara moja kwa mwaka.
Mbali na watu hao wa karibu kabisa
katika shughuli hiyo, pia mama na dada
yake walikuwepo kumpongeza kwa
kutimiza miaka hiyo ambayo inaendelea
kutimiza safari ya kuelekea uzeeni.
Hata hivyo, hafl a hiyo ilionekana
kumchanganya Jennifer baada ya
mumewe kufanya hivyo kwa kumshtukiza
licha ya kupiga pamba za nguvu ambazo
zilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu
pamoja na nywele zilizoonekana kuwa
kivutio kwa washiriki wa sherehe hiyo.
Mashabiki wa mwanamuziki huyo
baada ya kusoma habari zake mtandaoni,
walitoa maoni yao na kusema kuwa
mwanadada huyo ameonekana kuzeeka
na kumshauri atafute watoto wengine
mbali na mapacha wawili alionao kwa
madai kuwa hawamtoshi.
KUZALIWA KWAKE
Jennifer Lopez alizaliwa Julai 24.1969
Ni muimbaji na muigizaji mzaliwa wa
Marekani pia anajishughulisha na uandaaji
wa muziki kama ‘Record Producer’
Baada ya kuzaliwa alilelewa katika eneo
la Bronx jijini New York. Wazazi wake ni
Guadalupe Rodriguez na David.
Jennifer ni mwenye imani ya kanisa
katoliki. Shule aliyosoma ni Preston.
KUANZA MUZIKI
Alianza muziki rasmi akiwa na umri wa
miaka 19, huku akiwa anacheza katika
kumbi za usiku huko Manhattan, wakati
huo huo alikuwa akifanya kazi katika ofi si
ya sheria.
Pia alikuwa akifanya kazi ya kucheza
muziki kwenye video mbalimbali za
wasanii wakubwa akicheza shoo, aliwahi
pia kucheza kama mnenguajia wa Janet
Jackson’s kwenye video yake ya ‘That’s
The Way Love Goes’.
Muvi ambazo amewahi kucheza akiwa
na umri mdogo.
Alicheza fi lamu ya kwanza mwaka
1995 My Family, ikifuatwa na Alongside
Wesley Snipes in Money Train, nyingine
aliyowahi kucheza ni Blood and Wine
ikiwa ni mwaka 1997.
Filamu alizocheza ni nyingi na
nilizoorodhesha hapo juu ni baadhi tu.
Amewahi kuchaguliwa kama muigizaji
bora mwaka 1997 katika zawadi za Golden
‘Globe award’ ikiwa ni mara ya kwanza
baada ya kuingia katika tasnia ya uigizaji.
MAISHA BINAFSI YA JENNIFER
LOPEZ:
Aliwahi kuolewa na Ojani Noa mwaka
1997 lakini waliachana na kupeana talaka
kabla ya kutimiza miezi 12.
Mwaka 1990, Jennifer Lopez alikuwa na
uhusiano wa mapenzi na staa wa muziki wa
Hip hop, Sean Combs (Puff Daddy). Hata
hivyo, uhusiano wao haukudumu sana
kwani waliachana baada ya kushikiana
bastola kwenye ugomvi uliotokea huko
Manhattan kwenye ukumbi wa starehe
nyakati za usiku .
Ndoa ya pili ya Lopez ni ile aliyofunga
na mnenguaji Cris Judd, ndoa hiyo iliishia
pale Jennifer alipoanza uhusiano na
muigizaji Ben Affl eck.
Yeye na Ben Affl eck walivalishana pete
ya uchumba November 2002 na ndoa
ilikuwa ifungwe mwaka 2003, lakini ndoa
hiyo ilisitishwa ghafl a.
Baada ya hapo Lopez akaolewa na Marc
Anthony, ambaye alikuwa akifanya naye
muziki kipindi cha nyuma na ndoa yao
ilifungwa mwaka 2004 ambayo ilijibu
Februari 2008 baada ya kupata watoto
mapacha.
Aelekea uzee sasa, wadau wamshauri kutafuta watoto wengine
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment