.

.

Saturday, August 22, 2009

Miaka 39 ya Maria Carey


Maria aamua kuendeleza
bifu na Eminem
Amtungia wimbo na
kuvaa uhusika wake
Manamuziki wa pop nchini
Marekani Mariah Carey
ameamua kujikita rasmi
katika bifu na msanii
mwenzake Eminem ambaye
amekuwa akimuimbia nyimbo
mbalimbali za kumkashfu.
Kwa mujibu wa mtandao
mmoja nchini humo umedai
kuwa mwanamama huyo
kwa sasa ametunga wimbo
unaitwa ‘Obsessed’
ambao amevaa uhusika
wa sura mbalimbali
ikiwemo sura ya kiume
ambayo wadau wanadai
kuwa mwanamuziki huyo
amemuimbia Eminem ambaye
amekuwa akijaribu kumchafua
mara kwa mara.
“Hebu angalia sura ya kiume
ambayo ameitumia inafanana na
ya Eminem na hata ujumbe ambao
amekuwa akiutumia kwenye nyimbo
zake moja kwa moja una mlenga
mwanamuziki huyo.
Mwanamuziki Eminem naye analitaka
bifu kwani ametangaza kutoa picha za
utupu za malkia huyo huku akitishia
kuzisambaza kwenye mitandao
mbalimbali nchini humo.
Eminem na Maria wamejiingiza kwenye
malumbano kwa muda wa miaka sasa na
mwaka huu bifu lao limeonekana kuzidi
kuvuta kasi baada ya Maria kuamua
kumjibu kwa nyimbo na mifano hasa
pale alipobadili sura na kuwa mwanaume
aliyefanana na Eminem.
Eminem amemuimba vibaya
mwanamama Mariah katika nyimbo
yake inayoitwa “The Warning,” akiwa
amedhamiria kuharibu kabisa ndoa ya
Maria na mumewe Nick Cannon kwa
kupitia picha hizo ambazo anataka
kuzitoa ikiwa ni pamoja na ujumbe
wa sauti wa mariah Carey ambao anao
kwenye mashine ya kuongelea.
Hata hivyo minongono iliyoenea
mitaani inadai kuwa Malkia huyo
wa Pop na Eminem walikuwa na
uhusiano mwaka 2001 na baada ya
kuvunja uhusiano huo ndipo bifu
kubwa kati yao lilopoibuka.
KUZALIWA KWAKE:
Mariah Carey alizaliwa mach 27,
1970 huko Huntington, kisiwani
New York Marekani akiwa ni mtoto
wa tatu na wa mwisho wa Patricia
Carey (Née Hickey), aliyewahi kuwa
mwanamuziki na baba yake ni
Alfred Roy Carey akiwa ni Afrikasti
wa Kivinezuela.
Jina la Carey alilitoa kwa babu yake
mzaa baba baada ya kutoa wimbo wa
“They Call the Wind Mariah”.
Baba na mama Carey walitengana
akiwa na umri wa miaka mitatu tu.
Kwa sasa Maria ni mke wa mtu na
anaelekea kutimiza miaka Arobaini
baada ya kusherehekea miaka 39 Mach
27 mwaka huu.
Eminem aahidi kutoa
picha zake za utupu
Weekly

No comments:

Post a Comment