.

.

Wednesday, November 4, 2009

Rubi Tamthilia mpya usikose kuisoma kila wiki


Sehemi ya kwanza ya tamthilia ya Rubi…

Rubi na Maribel wanakuwa marafiki wakubwa. Maribel na rubi wanasoma shule moja . Maribel anakuwa na tatizo kwenye mguu wake.baada ya kutoka shule, maribel anaamua kumpeleka rafiki yake kwenye nyumba yake kubwa, Rubi anashangazwa na nyumba ile na kuwa na wivu ambao anauweka moyoni na kuwa siri yake. Maribel anakaa nay echini na kumpatia siria yake ya mapenzi ambapo anamwambia kuwa anampenda mwanaume anayeitwa Hector na kumuweka wazi kuwa amefahamiana naye kupitia mtandao wa Intanet, akamwamelezea kuwa mwanaume huyo anaishi New York kwa muda na hivi karibuni atakuja Mexico.

Rubi yeye anaishi karibu na hapo na anaishi katika maisha ya kimaskini pamoja na baba yake na dada yake anayeitwa christina ambaye anafanya kazi kwa nguvu kuhakikisha Ruby anamaliza masomo yake.

Hector mwanaume anayependwa na Maribel anakuwa tayari kusafiri na rafiki yake anayeitwa Alejandro kwenda Mexico. Rafiki huyo wa Hector ni maskini wakati Hector akiwa tajiri, Hector akiwa anajiandaa na safari anatuma cheni kwa maribel na ujumbe ukimwambia kuwa atafika siku chache zijazo huko Mexco wanakoishi Maribel na rafiki yake Rubi.

maribel baada ya kupata ujumbe na cheni anafurahi sana na kumwambia rafiki yake rubi, lakini baada ya kumwambia hivyo akamuuliza kama Hector anafahamu juu ya ulemavu wake, maribel akamwambia hapana kisha swali hilo likaanza kumchanganya kwani alikuwa akiogopa kusema swala hilo kwa Hector kwasababu aliogopa kumpoteza kwasababu ya ulemavu wake.

Maribel anampa ofa Rubi ya kitu chochote anachotaka hasa katika nguo zake,pamoja na zahabu kama atataka. Rubi anamwambia dada yake kuwa ana wivu juu ya maribel kwasababu ana kila kitu wakati yeye hana chochote...

Rubi pia anakuwa na wivu na dada yake mkubwa christina. Maribel na Rubi wanakwenda uwanja wa ndege kumpokea Hector na rafiki yake Alejandro, Rubi anaonekana kuvutia zaidi kutokana na nguo yake ya pink ambayo alikuwa amevaa ambayo alipatiwa na maribel.

Wanapofika uwanja wa ndege Maribel anakaa mbali Rubi anakwenda kumuangalia Hector, alipomuona tu Hector akambusu kwenye shavu na kumuuliza iwapo anamkumbuka.

“don't you remember me ‘unanikumbuka’? ".

Endelea kusoma uhondo wa Tamthilia hii….


Rubi akiwa katika pozi...
Wadau tamthilia hii ina mafunzo wenye 'mashost' wenu waangalieni mara mbili mtakosa waume

No comments:

Post a Comment