Elizabeth apokelewa kwa shangwe Dar!
ALIYEKUWA mshiriki wa Tanzania katika shindano la Big Brother Afrik, Elizabeth Gupta juzi alipokelewa kwa shangwe jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Afrika Kusini.
Mshiriki huyo alitolewa wiki iliyopita baada ya kuingizwa kwenye mchujo na Edward wa Namibia ambaye alimuweka kwenye mchujo badala ya rafiki yake mkubwa Mzamo ambaye hushirikiana naye katika kuvuta sigara.
Pamoja na kutolewa kwa Elizabeth, watanzania wamempongeza kwa kitendo chake cha kuepuka vishawishi vya ngono na kufikisha siku 63 ndani ya jumba la Big Brother.
Mashabiki wengine waliofika Uwanja wa Ndege kumlaki Elizabeth, walilalamikia shindano hilo na kuongeza kuwa hawakuelewa kilichomtoa mtanzania huyo mapema kwani alishiriki ipasavyo shindano hilo.
Elizabeth anatarajiwa kupongezwa na watanzania wenzake leo katika ukumbi wa klabu ya Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Elizabeth na Sister Doi katika picha ya pamoja uwanja wa Ndege
Elizabeth akiwa katika pozi uwanja wa ndege alipotua jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment