.

.

Monday, November 23, 2009

Hongera kaka karashani,karibu nyumbani wifi Debora

Madada zake, Anastazia, Lilian na Mariath nao walikuwepo

Hivi ndivyo harusi ya karashani ilivyosherehekewa na ndugu na jamaa kwa furaha shangwe na vigeregere hongera kaka!

Karashani akipewa majukumu Rasmi
Dada yake karashan, Mgeni Hassan akifungua shampagne kwa furaha kama zawadi ya kwanza kwa kaka yake
Mtoto wake Karashani Evon a.k.a Furaha akifurahia harusi ya mjomba wake
Dada yake Karashani Achi akiwa na mumewe Faridi ndani ya sherehe hiyo
Karashani baada ya kupewa majukumu na kaka yake Emili, mkewe Debora alimshangilia kwa furaha na kupiga makofi

Philbet Karashan a.k.a Jamal alipopata jiko

wazazi wake wakimpongeza kwa wimbo baada ya kupewa majukumu na kaka yake Emil
Kaka yake Emil akijiandaa kumkabithi majukumu ya familia kama mwanaume
Karashani akipeleka keki kwa wakwe zake akisindikizwa na mkewe Debora
Karashan akimlisha keki mkewe Mpendwa Debora siku yao maalumu
Karashani akifikilia jinsi atakavyomnywesha mkewe mpendwa shampagne

Thursday, November 12, 2009

Mapokezi ya Elizabeth wa BBA Dar

Elizabeth apokelewa kwa shangwe Dar!

ALIYEKUWA mshiriki wa Tanzania katika shindano la Big Brother Afrik, Elizabeth Gupta juzi alipokelewa kwa shangwe jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Afrika Kusini.

Mshiriki huyo alitolewa wiki iliyopita baada ya kuingizwa kwenye mchujo na Edward wa Namibia ambaye alimuweka kwenye mchujo badala ya rafiki yake mkubwa Mzamo ambaye hushirikiana naye katika kuvuta sigara.

Pamoja na kutolewa kwa Elizabeth, watanzania wamempongeza kwa kitendo chake cha kuepuka vishawishi vya ngono na kufikisha siku 63 ndani ya jumba la Big Brother.

Mashabiki wengine waliofika Uwanja wa Ndege kumlaki Elizabeth, walilalamikia shindano hilo na kuongeza kuwa hawakuelewa kilichomtoa mtanzania huyo mapema kwani alishiriki ipasavyo shindano hilo.

Elizabeth anatarajiwa kupongezwa na watanzania wenzake leo katika ukumbi wa klabu ya Bilicanas jijini Dar es Salaam.

Elizabeth na Sister Doi katika picha ya pamoja uwanja wa Ndege

Elizabeth akiwa katika pozi uwanja wa ndege alipotua jijini Dar es salaam

Saturday, November 7, 2009

Wiki ya shwahili hood ilifanya kama ifuatavyo

Mustafa Hassanali katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanamitindo kutoka nchini Kenya.
Mr. Dar Handsome 2007-08, Mwinyi Ahmed, akiwa juu ya jukwaa kuonyesha moja ya vazi katika ukumbi huo.
Richa Adhia, Miss Tanzani 2007-08, akiwa jukwaani tayari kuonyesha vazi alililokuwa amevaa katika maonyesho hayo.
Miss Tanzania 2008-09, Nasreen Karimu, akikatiza jukwaani kuonyesha baadhi ya mavazi.
Mwanamitindo Miriam Odemba (kulia), akiwa kwenye pozi la pamoja na Killy Janga, Miss Utalii 2006-07, muda mfupi baada ya kuwasili kwenye tamasha hilo.

Wednesday, November 4, 2009

Na hii nyingine Shades Of Sin




Ujauzito wa Barbara unamshtua Paco na hakuweza kuachana na Barbara. Dodô anachanganywa na Preta. Paco anampigia simu Preta, lakini Dodô hamruhusu kupokea ile simu. Dodô anajaribu kumlazimisha Petra, lakini Preta anakimbilia kwa Helinho ili amsaidie kumuwekea ulinzi.

Lita anamwambia Preta kumsahau Paco. Marafiki wawili wanamwambia Paco kwamba Afonso alimesambaratisha msitu kwa ajiri ya kujenga. Paco anasoma malalamiko juu ya Afonso,ambayo Afonso anaona kwenye TV. Ulisses anakiri kwa Apolo kwamba alitumia pesa zote kwa mwanamke ambaye anampenda. Apolo anashauri yeye na Ulisses waende likizo. Verinha anapata nguvu pale Barbara anapomwambia kuwa ni mjamzito. Afonso anamhakikishia Paco kwamba hawezi kuusambaratisha msitu, lakini kisha anatoa amri kuwa msitu usambaratishwe kisiri bila mtu yoyote kugundua. Edilásia anajaribu kukopa pesa za Ulisses, lakini hawezi kukubari. Paco anagundua baba amesambaratisha msitu na kuchanganyikiwa. Germana anatoa ushauri kwa Paco na kumwambia kuwa aende kwa mwanamke anayempenda. Barbara anafanikiwa kuipata tiketi ya Paco na kuuliza ni kwanini anataka kurudi Maranhão je Paco atamjibu nini?Endelea kupata uhondo.

Sehemu ya Tatu 3:

Jumatano Wednesday, 01/28/2004 – Paco anarudi Maranhão - Paco anamdanganya Barbara kwamba anarudi kule sababu ya biashara. Anahisi kuwa Paco anataka kuusitisha uhusiano wake amwachii kuongea chochote. Preta anakuwa na hasira baada ya kukosa kabisa habari za Paco. Barbara anajaribu kufatilia kutoka kwa Felipe kwanini Paco anarudi Maranhão, lakini anamjibu kwamba hajui chochote. Abelardo anaweka wazi kwa Edilásia kwamba yule Ulisses ametumia pesa zake zote kwa ajiri ya mw anamke ambaye anampenda. Ulisses anamuomba Verinha kumrudishia mkufu wake ambao alimpatia. Anachanganyikiwa na kuachana na yeye. Paco anampigia simu Preta, lakini Lita anamwambia kuwa hataki kuongea naye. Edilásia anamshauri Ulisses. Barbara anamwambia Afonso kwamba Paco anakwenda safarini. Afonso anatoa oda kwa Felipe kumzuia Paco kuingia kwenye ndege. Edilásia anatengeneza picha nyingine pale alipogundua kuwa Apolo na Ulisses wanataka kusafiri. Felipe awasiliani na Paco kwa wakati. Huko Maranhão, Paco anamwambia Helinho kwamba anamtafuta Preta. Ulisses na Apolo wanaondoka kwenye boat. Barbara anataka kwenda São Luis, lakini Kaike anamfanya atengeneze wazo fulani. Helinho anamchukua Preta na kumpeleka kwa Paco.

Sehemu ya 4: Alhamisi AMANI

Preta anakubari kuolewa na Paco – Paco na Preta wanabusiana kimahaba. Helinho na Cezinha wanaondoka huku wakilia. Barbara anajaribu kumshawishi Germana amwambie Paco alipo lakini anashindwa. Germana anamwambia Barbara kwamba yeye si mwanamke sahihi kwa Paco. Afonso anajaribu kumtuma Felipe kwenda Maranhão kumtafuta Paco. Felipe anakataa kwenda, akimchanganya Afonso. Paco anamwambia Preta kumuoa, lakini anaomba ampatie muda ili afikilie zaidi juu ya suala hilo. Edilásia anachanganyikiwa pale anapogundua kuwa Tina amesababisha ugomvi kati ya Apolo na Thor.

Ulisses na Apolo wanagundua kuwa wamesahau kuweka mizigo kwenye boat pamoja na maji na chakula. Barbara anafanya uchunguzi kwenye nyumba ya Paco na kugundua picha ya Preta,kitendo kinachopelekea yeye kuchukua uamuzi wa kwenda São Luis. Kaike anaamua kwenda naye. Barbara anapofika huko anakwenda sehemu ya madawa ya Preta na kumuuliza Lita kama anamfahamu Paco.Lita akakataa kumjua kijana huyo. Paco anaweka wazi kwa Preta kwamba amejiweka kwa mwanamke ambaye hampendi. Preta anakubari kuolewa na Paco, ambaye anampatia pete aliyopewa na mama yake. Barbara anafika na bahati mbaya anamuona Paco na Preta wakibusiana.

Sehemu ya 5: Ijumaa.

Kaike na Barbara wanapanga na kisha wanakwenda sehemu ambayo Paco amefikia Barbara anamfata Paco na Preta na kugundua kuwa wapenzi hao wanampango wa kuoana. Verinha na Eduardo wanaumia baada ya kukosa pesa. Barbara anamuomba Kaike amsaidie kumrudisha Paco. Apolo na Ulisses wanatua ufukweni. Thor anamwambia Edilásia kwamba anakwenda kuangaika na kumuomba amtengenezee supu ambayo itampa nguvu.

Preta anamwambia Helinho kwamba anaolewa. Afonso anatoa maoni kwa Italo kwamba ni furaha kuwa na mtoto wa kiume ambaye anampenda. Paco anampigia simu Barbara na kujaribu kuvunja uhusiano naye,lakini alipopokea simu akajifanya kuwa mawasiliano ni mabaya. Lita anaduwaa pale Preta alipomwambia kuwa Paco amemuomba kumuoa. Edilásia anaandaaa supu ya Thor. Kaike anayasoma maisha ya Preta. Apolo na Ulisses wanagombana na msichana ufukweni akiwa na mume wake. Thor anapigwa na adui yake. Edilásia, bila kujua ni kwanini haikupedwa zaidi, anaingiza pete yake kumuokoa kijana wake. Barbara anaingia kwenye chumba cha Paco.

Sehemu ya 6: Jumamosi.risasi

Mshtuko unatokea kwenye pati ya kuvarishana pete – Paco anashangaa kumuona Barbara. Dodô anaomba kuongea neno juu ya Preta. Edilásia anampatia Thor supu nyingi zaidi, anashinda mechi. Dodô anasisitiza Preta arudi kwake lakini anashikataa. Kaike anaona kila kitu tokea mbali. Eduardo anatoa ushauri kwa Verinha kwamba wamesahau michoro ya kuuza. Barbara anajifanya anaumwa hivyo Paco ataachukua jukumu la kumuangalia. Preta anawakubari wa geni kwenye pati yake. Edilásia anamfata Thor ajiapize kuwa ataachana na Tina, lakini anadanganya. Ulisses na Apolo wanafika kwenye bandari mpya na kuanza kugombana. Verinha anachukua picha moja wapo ya mchoro wa Afonso. Preta anamkaribisha Helinho kuwa msimamizi wake kwenye harusi yake. Luis anamuona Ulisses na Apolo wakigombana na kuwaomba kama wanataka kutoa somo la mchezo wa mieleka. Paco anagundua kuwa amechelewa kwa ajiri ya pati, lakini Barbara hawezi kumuacha akaondoka. Preta anachanganyikiwa baada ya kuona Paco amechelewa. Abelardo anatangaza kwamba anataka kuwa mpambaji mwenye ujuzi na Edilásia anazimia.Preta anampatia kijana mdogo ujumbe kuwa amwambie Paco kwamba atofika kwenye pati.

Sehemu ya 7: Jumatatu

Preta anamsamehe Paco – Helinho anamliwadha Preta kutokana na kitendo kilichotokea. Kaike anamwambia Barbara kwamba mpango wao umefanikiwa. Paco anakwenda nyumbani kwa Preta anamtafuta, lakini Lita anamwambia asionekane tena hapo nyumbani. Preta anaamua kutoa maelezo kwa Paco. Barbara anaacha ujumbe kwenye kioo cha chumbani kwa Paco kwa ajili ya Preta kuona. Preta anakasirika pale anapoona ujumbe na kuacha pete aliyopewa na Paco mwisho wa kitanda. Gari zuri ambalo analizuza Afonso linapita mtaani kwa akina Preta and the bandit take $5 million in gold. Cezinha analiona. Paco anakasirika pale anapoona Preta amerudisha pete. Afonso anachanganyikiwa pale anapogundua kuachwa kwa pete ile. Wezi wanakimbilia mbali kutoka Maranhão. Apolo na Ulisses wanaanza kupata somo la mieleka. Edilásia anambembeleza Abelardo asiwe msanii wa kupamba. Paco anamuelezea Preta kwamba mwanamke aliyeacha ujumbe kwake ni mpenzi wake wa zamani. Preta anamsamehe Paco. Verinha na Eduardo search for a forger. Wezi wanaomba kukodisha boti ya Ulisses. Paco anamkuta Barbara kwenye nyumba ya Preta.

usikose kufatilia wiki ijayo

Rubi Tamthilia mpya usikose kuisoma kila wiki


Sehemi ya kwanza ya tamthilia ya Rubi…

Rubi na Maribel wanakuwa marafiki wakubwa. Maribel na rubi wanasoma shule moja . Maribel anakuwa na tatizo kwenye mguu wake.baada ya kutoka shule, maribel anaamua kumpeleka rafiki yake kwenye nyumba yake kubwa, Rubi anashangazwa na nyumba ile na kuwa na wivu ambao anauweka moyoni na kuwa siri yake. Maribel anakaa nay echini na kumpatia siria yake ya mapenzi ambapo anamwambia kuwa anampenda mwanaume anayeitwa Hector na kumuweka wazi kuwa amefahamiana naye kupitia mtandao wa Intanet, akamwamelezea kuwa mwanaume huyo anaishi New York kwa muda na hivi karibuni atakuja Mexico.

Rubi yeye anaishi karibu na hapo na anaishi katika maisha ya kimaskini pamoja na baba yake na dada yake anayeitwa christina ambaye anafanya kazi kwa nguvu kuhakikisha Ruby anamaliza masomo yake.

Hector mwanaume anayependwa na Maribel anakuwa tayari kusafiri na rafiki yake anayeitwa Alejandro kwenda Mexico. Rafiki huyo wa Hector ni maskini wakati Hector akiwa tajiri, Hector akiwa anajiandaa na safari anatuma cheni kwa maribel na ujumbe ukimwambia kuwa atafika siku chache zijazo huko Mexco wanakoishi Maribel na rafiki yake Rubi.

maribel baada ya kupata ujumbe na cheni anafurahi sana na kumwambia rafiki yake rubi, lakini baada ya kumwambia hivyo akamuuliza kama Hector anafahamu juu ya ulemavu wake, maribel akamwambia hapana kisha swali hilo likaanza kumchanganya kwani alikuwa akiogopa kusema swala hilo kwa Hector kwasababu aliogopa kumpoteza kwasababu ya ulemavu wake.

Maribel anampa ofa Rubi ya kitu chochote anachotaka hasa katika nguo zake,pamoja na zahabu kama atataka. Rubi anamwambia dada yake kuwa ana wivu juu ya maribel kwasababu ana kila kitu wakati yeye hana chochote...

Rubi pia anakuwa na wivu na dada yake mkubwa christina. Maribel na Rubi wanakwenda uwanja wa ndege kumpokea Hector na rafiki yake Alejandro, Rubi anaonekana kuvutia zaidi kutokana na nguo yake ya pink ambayo alikuwa amevaa ambayo alipatiwa na maribel.

Wanapofika uwanja wa ndege Maribel anakaa mbali Rubi anakwenda kumuangalia Hector, alipomuona tu Hector akambusu kwenye shavu na kumuuliza iwapo anamkumbuka.

“don't you remember me ‘unanikumbuka’? ".

Endelea kusoma uhondo wa Tamthilia hii….


Rubi akiwa katika pozi...
Wadau tamthilia hii ina mafunzo wenye 'mashost' wenu waangalieni mara mbili mtakosa waume