.

.

Thursday, October 1, 2009

DONDOO NYINGINE ZA TIBA ASILIA NI KAMA ZIFUATAZO






Juice ya nyanya:
Juisi ya nyanya ukichanganya na chumvi kidogo pamoja na pili pili ni dawa homa ya manjano ‘Jaundice’ inafaa kunywewa asubuhi kabla ya kifungua kinywa.

Tunda la Mzaituni:
Mafuta ya mzaituni ni dawa kwa ajiri ya kuondoa vipele vya joto unapaka lile eneo lililoathilika. Pia ukipakaa ngano eneo lililoathirika na vipele vya jasho inatibu.

Zabibu kavu:
Ukila zabibu kavu kwa wingi ni tiba kwa wale wanaotaka kuongeza uzito wa mwili.

Kiazi mbatata:
Kiazi mbatata ni tiba kwa mabaka au madoa doa yanayokuwa kwenye mwili hasa usoni unakata kipande chembamba na kukiweka sehemu iliyoathirika.

Ndizi mbivu:
Ndizi mbivu ni nzuri kwa kutibu madonda ya tumbo.

No comments:

Post a Comment