.

.

Saturday, June 12, 2010

Marichuy anagundua mchezo mchafu anaofanyiwa na Stefano.

Alhamis

Marichuy anagundua mchezo mchafu anaofanyiwa na Stefano. Stephanie anamkuta Marichuy ndani ya dimwi la kuogelea. Stephanie anachukizwa na muonekano wa Marichuy. Marichuy, anashangaa ni kwanini Stephanie anamfanyia vitimbi na kumuuliza, anajibu kwamba hawezi kuwa na msimamo hata hivyo. Patrick, Cecilia na Isabella wako na Marichuy pembeni. Patricio anamlazimisha Marichuy kumwambia cheni ya Stephanie iko wapi, hakujua nini aliongea. Patricio anamwambia Marichuy kuwa ni muongo, na kusisitiza kuwa ameiba cheni kama alivyoiba pesa, Marichuy akajibu kuwa muongo ni yeye, baada ya majibu hayo Patricio akampiga kofi. Cecilia anamuomba Marichuy akae chumbani kwake, pamoja na kumuambia hivyo Patrick yeye akajiapiza kuwa lazima swala hili alifikishe kwenye mkono wa sheria.

Huko kanisani, Edward anakuwa na hasira kwasababu msichana wake hajaficha. Francisco anafika kanisani na kumwambia Juan Miguel kuwa hakutakuwa na harusi kwasababu ya Elsa. Elsa anafika kwa Nelson akiwa na nguo ya harusi, hakuwa amejifunika wala kuwa na maua akalia na kumkumbatia Nelson kwa uchungu. Estefania anaangalia mkufu kisha anafungua mlango wa Marichuy. Stephanie anapofungua Marichuy anaona mkufu. Marichuy anamuuliza Stephanie kila kitu kimefanywa ili kumuunguza yeye, lakini akamwambia kuwa hatokubari kwani atakwenda naye kwa wazazi wake kwenda kusema ukweli. Je Itakuwaje usikose wiki ijayo hapa hapa amani.

Icheki Tamthilia hii kupitia Sisterdoi.blogspot.com

Ijumaa July 11, 2008 - Juan Miguel anamwambia Patricio kwamba ataondoka na Marichuy nyumbani kwake.

"Sebureni kwa Velarde Juan Miguel, Patricio, Cecilia na Stephanie wanakutana. Patricio anawaambia kuwa Marichuy ana mambo mawili anatakiwa kuchagua kuondoka nyumbani kwake na kwenda mtaani au kwenda jela. Juan Miguel anamwambia Patricio kwamba Marichuy ataondoka naye, Stephanie kusikia hivyo anapandwa na hasira. Juan Miguel anakwenda nyumba ni kwake na Marichuy. Onelia anamwambia Juan Miguel kwamba hawezi kukaa chini ya paa moja na Marichuy Miguel akajibu kwamba yeye ndo ameshaamua hivyo atake asitake Marichuy atakaa ndani ya nyumba hiyo.

Baada ya kutulia ndani ya nyumba ya Miguel kwa muda wa dakika tano, Marichuy, Vicente, Rocio, Amador, Vicente, Becky, Elsa na Nelson wanakutana kwenye paty ambako Marichory na Rocio wamekwenda kwa kutoroka. Rocio anacheza na Vincent na kujifunza kuvuta sigara, ambaye anasema kuwa amependa na anataka kuwa mshirika. Becky anafungua mlango na kumkuta Juan Miguel ambaye anaingia kwenye party, anamkuta Eloy na Marichuy wakicheza muziki huku Rocio akibusiana na Vicente. Juan Miguel anamvuta Marichuy na Rocio na kuondoka nao. Amador anapomuona Miguel anamsema vibaya kuwa ameingia kumchukua Marichuy.

Kwenye bustani ya nyumbani Juan Miguel anakutana na Marichuy wanakaa kwenye kibaraza cha ghorofani wakiangalia mawingu, Marichuy anashindwa kuzuia hasira zake. Juan Miguel anamsogelea na kumzuia kuangalia juu akajaribu kuongea naye. Juan Miguel anamwambia Marichuy kuwa anajisikia vibaya file alivyomfanyia. Marichuy anamwambia Juan Miguel kuwa anampenda,Miguel akamuangalia kwenye midomo yake,jinsi ilivyogawanyika. Juan Miguel na Marichuy wakabusiana.

Je itakuwaje endelea….

Jumatatu July 14, 2008 - Juan Miguel anamwambia Marichuy kwamba mchungaji amwemwambia amuelezee juu ya ndoto yake. Marichuy alipoambiwa hivyo akakaa mbali na Juan Miguel na kumuangalia kama mtu aliyeshtuka hivi, akaomba msamaha na kujaribu kumshika,lakini Marichuy akamwambia aondoke. Ofisini mapokezi Juan Miguel na Estefanía wanakutana na Israel ambaye alikuwa akifika. Israel anamuuliza Stephanie kama bado anahisi kuwa ataolewa na Juan Miguel, akasema hapana anajipenda yeye mwenyewe. Stephanie anambusu Israel kwa pozi, ambaye haoneshi kukasirika. Israel anaonesha kumkubaria Stephanie, ambaye anampiga kofi kwa hasira .Mlango wa kanisani unafunguliwa mchungaji Anselmo, anashangaa kumuona Juan Miguel. Juan Miguel anamwambia mchungaji Anselmo kuwa anataka kuongea na yeye kuhusiana na Marichuy.

Tuesday July 15, 2008 - Marichuy anakumbuka maisha yake ya zamani. Juan Miguel anaongea na Marichuy ofisini kwake. Marichuy anamwambia Juan Miguel kilichotokea, akamwambia kuwa yeye sisi mjinga, mara mlango ukafunguliwa na Eduardo. Baada ya Marichuy kwenda nyumbani Juan Miguel akamwambia Eduardo kuwa alidhani Marichuy atamwambia kitu chochote. Marichuy. Juan Miguel anaongea na mchungaji Anselmo. Mchungaji anamwambia Miguel kwamba anajua kwa sasa majuto yake yanakuwa makubwa kwasababu anampenda Marichuy. Juan Miguel na Marichuy wanachati wakiwa kitandani, Miguel anamwambia kuwa hawezi kumchukia, lakini akasisitiza kwamba watafanya jambo pale atakapomwambia kosa liko wapi, hakutaka kumuangalia machoni, hata hivyo Eduardo hakarudi. Juan Miguel akamchukua Marichuy na kumuweka karibu na kukiri kwamba anampenda kama mwanaume mwingine anavyoweza kumpenda. Juan Miguel anamsisitizia Marichuy kuwa anampenda. Marichuy anakuwa nje kwenye bustani , Juan Miguel anamkumbatia, lakini Marichuy anamwambia kuwa hawezi kuwa naye karibu kwasababu hamtaki mtu amshike, Juan Miguel anamuuliza kama walipobusiana alijisikiaje na kumuomba arudie ili aone. Juan Miguel akambusu tena Marichuy kwenye midomo yake, ambaye alikuwa akianza kujiachia na kuvuta hisia lakini alishindwa baada ya kuvuta kumbukumbu kuwa yule ni mpenzi wa Stephanie na yeye anajua kuwa wao ni wapenzi.

Jumatano :July 16, 2008

Juan Miguel anamwambia Marichuy hampendi Steff, anampenda yeye. Onelia na Juan Miguel wanakunywa chai,Onelia anakuwa anamuongelea vibaya Marichuy na tabia zake.

Juan Miguel anamwambia Onelia kuwa yeye hamtetei mtu wa mtaani tu bali anamuhifadhi mtu ambaye ni muhimu sana kwake.

Juan Miguel anamuomba Onelia amuheshimu Marichuy kwasababu anataka kumuoa. Onelia anampigia simu Estefania na kumwambia kuwa Juan Miguel ana mpango wa kumuoa Marichuy. Adrian anakwenda kumuona Juan Miguel ofisini kwake, akaenda kumlalamikia kwa kitendo chake cha kutomuheshimu Marichuy na kumpatia haki yake.Marichuy anakwenda kwa Adrian kumlaumu kwa kile alichofanya ofisini kwa Miguel.

Marichuy anamuelezea Adrian kuwa Juan Miguel hajafanya kitu kibaya, hivyo akamuomba amuache peke yake na Juan Miguel. Juan Miguel anamwambia Marichuy kwamba hampendi Stephanie anampenda yeye na anataka kumuoa yeye, Marichuy anapatwa na mshtuko kusikia hivyo. Juan Miguel akambusu Marichuy mdomoni baada ya kumwambia hivyo, kisha akamkumbatia na kumuweka mikononi mwake. Juan Miguel na Patrickwanaingia katika ugomvi mkubwa. Juan Miguel anamwambia Patricio hatomuoa mtoto wake kwasababu mwanaye anampenda Marichuy.

***

Alhamis.

Miguel na Marichuy wanaamua kuishi kwenye nyumba moja huku mama mkwe wa Miguel, Onelia anaweka kipingamizi lakini watu hawa wanamua kulazimisha na kuishi je watavumilia hisia zao? Endele kusoma Tamthilia hii ya kusisimua.

Baada ya Juan Miguel kumwambia Patricio kwamba hawezi kumuoa mtoto wake kwasababu hampendi Marichuy, Stephanie anasema, anatishia kwa kusema kuwa kati ya Juan Miguel au Marichuy mmoja atakuwa na furaha na mwingine atakuwa na machungu. Rocio na Vicente wanakaa kwenye kibaraza ‘balcony’ wakiangalia jiji.

Rocio anamwambia Vicente kwamba hajawahi kukaa pale na amevutiwa sana. Vicente anamkumbatia na kumbusu kwenye shingo yake, akasikia raha na kumwambia Vicente kwamba ni mara ya kwanza kupata furaha kama aliyonayo siku hii,kisha wakabusiana. Juan Miguel anafika kwenye geti la kuingilia jengoni ambako Ofisi yake ipo karibu kabisa na bench anakutana na gari ambalo analihofia, ambalo liko karibu kabisa na mlango wa jengo hilo. Bila kutarajia nje ya Benk anaona watu wakiwa wamejifunika sura huku wameshika siraha kwenye mkono wake, wakiwa kwenye marumbano kati yao na Polisi, wezi hao wakaanza kurusha siraha. Kati ya watu walioumia ni pamoja na Juan Miguel ambaye alipata maumivu makali na kuanguka chini. Kwenye office ya nyumbani kwa Gustavo Madrid anaingia Viviana na kumuuliza anamuonaje, ambaye anamjibu kuwa anaonekana mrembo, Viviana anahoji kama anaweza kuwa mwanamke mrembo basi ampatie kila kitu akajaribu kumbusu lakini akakataa, akaishia kukata tamaa. Juan Miguel yuko hospitali pamoja na Marichuy akamuuliza kama anaweza kuwa mke wake, Marichoy akachanganyikiwa hakujua la kufanya, Miguel akasisitiza swali lake mpaka mwisho wa siku akakubari. Furaha iliyoje Miguel akambusu mdomoni, kisha akamuomba msamaha kwa kitendo kile, akamuahidi kuwa hatorudia tena,Marichuy akatabasamu kama vile akisema kuwa ilikuwa itokee. Baada ya muda mchamche Stephanie akafika hospital kumuona Juan Miguel,ambaye amepata nafuu, Stephanie anamwambia Miguel kwamba haamini kama anaweza kuvunja uchumba wao Miguel anakiri kuwa anampenda Marichuy. Stephanie anakasirika na kumpiga kofi. Rocío na Marichuy wanakuwa na furaha kwa mapenzi mapya waliyonayo , hata hivyo Stephanie anasimama mbele yao akiwa na hasira na kuwatishia kuwa kati ya Juan Miguel au Marichuy mmoja wao hatokuwa na furaha,kwasababu maisha yatabadirika kwa kile walichokifanya. Stephanie baada ya maneno hayo akaondoka na kuwaacha Marichuy na Rocío wameshangaa.

Usikose wiki ijayo itaendelea….

Ijumaa July 18, 2008 - Juan Miguel anamwambia Eduardo kwamba hatosema ukweli kwa Marichuy.

Sehemu 30:

Juan Miguel anamwambia Eduardo kwamba ni bora asiseme ukweli kwa Marichuy kwasababu hatokubali amuoe, Edward akajaribu kumshawishi aseme ili asionekane ameanza ndoa na uongo. Rocio na Vicente wanapanda kwenye gari wakiwa wanaenda safari yao huko wanapata ajali mbaya na kuumia.

Onelia anakwenda ofisini kwa Juan Miguel na kutishia kwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka Mayita na

Marichuy. Hata hivyo baada ya kuona hana njia anaamua kumshawishi Mayita akamshtaki baba yake kwa kile alichokifanya. Marichuy anapokea simu, anagundua kuwa Dew amepata ajali. Onelia anasikia Marichuy akimwambia Juan Miguel hata akimuoa Mayita ataendelea kuwa mtoto wake na atakuwa kama alivyokuwa mama yake.

Monday July 21, 2008 - Rocío anaamka akiwa amelewa anashangaa kuona uso wake wote umezungukwa na bandeji.

Summary Chapter 31:

Rocío anaambiwa kuwa yuko hospitali, Edward anakuwa naye akimuangalia, Juan Miguel anaingia na kuuliza anaendeleaje. Rocío anafungua macho yake na kumuangalia Juan Miguel, akaweka mkono wake usoni na kushika uso wake akajikuta akilia sana. Mayita anatoka shule anaingiwa na mawazo kuwa amemuona mama yeke kwenye gari. Mayita anaamua kuingia mtaani, Mrs. Nesma haraka anamzuia, na kufikilia ni wapi Mayita amepata wazo la kuwa mama yake yuko mtaani wakati alishafariki. Mayita analia kwasababu hakuna mtu ambaye anamuamini kwamba amemuona mama yake, Juan Miguel anachanganywa na hali hiyo. Vincent bado amelala, anagundua kuwa yuko hospitali, baada ya nesi kuja na sindano. Daktari anatangaza kwa wazazi wa Vincent kwamba mtoto wao hawezi kutembea tena.

Jumanne July 22, 2008

Kwa jina la mungu, mchungaji Anselmo anawatangaza Juan Miguel na Marichuy kuwa mke na mume.

Summary of Chapter 32:

Mchungaji Anselmo, Juan Miguel, na Marichuy wanasubiri kwenye madhabau, Esther na Israel bila kutarajia wanatangaza kufika kuzuia ndoa ya Marichuy, ambaye anaingia kanisani akiwa mikononi mwa Eduardo. Mchungaji Anselmo anasema kama kuna mtu analo la kusema juu ya ndoa ya Juan Miguel na Maria de Jesus, aseme mapema. Hakukuwa na neno lolote hivyo mchungaji anawafungisha ndoa Maria de Jesus na Juan Miguel na kuwatangaza kuwa ni mke na mume. Juan Miguel na Marichuy wanakuwa katika mavazi ya usiku ya harusi. Marichuy analala kwenye mikono ya Juan Miguel, ambaye anaongea kwa upole kabisa na Marichoy wakati huo akipata hisia za kimapenzi zaidi. Juan Miguel anahisi hakuna mtu anayeweza kumsambaratisha na Marichuy na Marichoy moja kwa moja atamsamehe. Juan Miguel anambusu usoni Marichuy ambaye amelala na mwenye uso wa furaha. Nini kinafuata endelea…

Jumatano

Marichuy anamwambia Juan Miguel ni bora hasingesema ukweli. Juan Miguel na Marichuy wanabembelezana ufukweni, Miguel anamuuliza kama hakuwahi kumpenda na kukumbuka jinsi alivyokuwa na furaha alipokuwa mikononi mwake usiku.

Marichuy anamwambia Juan Miguel hatokaa akamsamehe. Marichuy anaanza kukimbia tena huko bichi, hata hivyo anajikuta amekosa nguvu na kuanguka mchangani ambapo anazimia, Juan Miguel anamfata. Marichuy anakwenda kujificha kwenye mapokezi ya hoteli iliyoko jirani, Juan Miguel anaamua kuingia hotelini ndani. Anasikia akiambiwa asubiri wakati akisubiri kufunguliwa, Marichuy anatoka nje na kujificha kwenye lango la kutokea.

Eduardo akiwa ofisini anamtembelea mgonjwa, anaaga kisha anaingia Stephanie akiwa amevaa vizuri. Marichuy anakuwa jirani akiongea na Candelaria, ambaye alikwenda kumuuliza kuhusiana na Juan Miguel akamjibu huku akifuta machozi.

San Román akiwa nyumbani, simu yake inaita na kupokelewa na Onelia,ambaye anasema kuwa hakuna majibu akihisi kuwa aliyepiga ni Viviana. Juan Miguel anakuwa kwenye mgahawa anaongea na Eduardo ambaye anampatia ufunguo wa nyumbani kwake kwasababu anasema kuwa hatohuhitaji, akamwambia kuwa Marichuy amemtenga baada ya kumwambia ukweli.

Hospitalini kunakuwa na watu wengi wa kutoka familia mbalimbali ambao wanasikia sauti ya Rocio akilia na kuogopa baada ya kustuka usingizini.

Alhamis

Juan Miguel, anaumia sana na kujaribu kujieleza kwa Marichuy. Je atakubari? Endelea kusoma…

Sehemu ya 34:

Juan Miguel, anaumia sana anajaribu kujieleza kwa Marichuy lakini anakuwa mkali na mwenye hasira, anasema kuwa alimficha ukweli wakati huo amejifungia bafuni akilia kwa uchungu, huku akiwa amechanganyikiwa na kufunika uso wake kwa mikono yake.

Elsa, na Beatriz haraka sana nao wanakimbilia chumbani kwa Rocio ambaye wanamkuta anafunua uso wake uliokuwa umejaa bandeji,na kusimama wima. Elsa na Beatriz wanaonekana wamefurahishwa na hali hiyo kuona kuwa Rocío ameweza kufunua uso wake. Juan Miguel anaendelea kuumizwa na Marichuy ambaye hataki kumsikiliza. Anakuwa na hasira,akimwambia kuwa alikuwa akimpa ushauri kwasababu ni yeye aliyefanya. Juan Miguel anamuomba sana. Marichy anamwambia kuwa asithubutu kufanya hivyo, akasema kuwa wametengana moja kwa moja, na kumwambia kuwa ajione kama mfu.

Marichuy anaamua kutoka nje, Juan Miguel anajaribu kumzuia, lakini mchungaji Anselmo anauzuia mkono wake. Marichoy akawa anamuangalia Miguel kwa chuki na hasira kisha akaondoka. Israel anakwenda hospital kumtembelea Dew, Stephanie anatoka na kumpatia habari kuwa alikuwa ni Rocio, Israel mwisho anaamua kumwambia hisia zake,kuwa anampenda. Stephanie akacheka kwa sauti ya juu, akamuoneshea dharau.

Ijumaa 25, 2008 –

Viviana anamwambia Mayita kwamba baba yake alijaribu kumuua.

Marichuy anakimbia akiwa amemkasirikia Juan Miguel anaamua kwenda kwa majirani, Miguel anakuwa na wasiwasi na ambaye amechanganyikiwa hataki mke wake aondoke bila kumsamehe, lakini kwa jinsi alivyomfanyia anaamua kuondoka eneo hilo.

Adrian anaenda kumuona mchungaji Anselm kanisani akitaka avunje ndoa ya Marichuy na Juan Miguel, mchungaji anakosa la kusema juu ya hilo. Viviana anamuona Mayita akimfatilia kwenye gari lake anamkimbilia na kumwambia kuwa baba yake alitaka kumuua, Mayita anashindwa kuamini habari anazoambiwa na mama yake. Je itakuwaje? Itaendelea wiki ijayoooo usikose

Saturday, May 22, 2010

Jinsi ya kumbana mpenzi/mume kiwembe

Hii ndo zana yenyewe ukishamvalisha unaibana na kufuli.. hebu angalia mfano hapo chini, wabaneni jamani wapenzi na wanaume zenu, wengine tulichelewa kuzijua zana hizi si wamekimbia.

Mashost katika vazi la ufukweni

Jeans mpya wadau

Ni kwa wenzetu wazungu lakini najua zikiingia kwa watanzania wapenda makuu watavaa tu...

Thursday, May 20, 2010

Top Ten Love Stories in World- Hadith za mapenzi 10 bora

10. Guinevere and Lancelot

Guinevere and Lancelot, 14th Century, English, literary. Based on the Arthurian legend, the doomed love between the gallant knight and beautiful queen caused the downfall of the Round Table.

9 Dante Alighieri and Beatrice

Dante Alighieri and Beatrice, 13th Century, Italian, historical. The writer met his muse when they were children. She inspired his greatest works although the pair never married. Beatrice is Dante’s guide through Paradise in “The Divine Comedy” and was the inspiration for 31 love poems, “La Vita Nuova.”

8 Cinderella and Prince

Cinderella and Prince Charming, 17th Century, French, literary. Based on Eastern European legends, this archetype of romantic love sent the message to women that if you keep your eyes open, someday your prince will come.

7. Rhett Butler and Scarlett O’Hara

Rhett Butler and Scarlett O’Hara, 20th Century, American, literary. Their fiery romance set amid the Civil War showed the pitfalls of pride and selfishness. He really did give a damn, and so did she.


6. Tristan and Isolde

Tristan and Isolde, 12th Century, English, French, German, literary. Based on an ancient Celtic legend as stubborn as the intertwined vines that grew over the lovers’ graves, the story of the knight who gave up his true love for a king has been told in many forms. Despite duty and other marriages, the lovers remain true to each other, and are reunited in death.


5 Robert and Elizabeth Barrett Browning

Robert and Elizabeth Barrett Browning, 19th Century, English, historical. Pale little Elizabeth bucked her dogmatic family and married a fellow poet. They spent their life in Italy amid sunshine and poetry, inspiring her to write a masterpiece, “Sonnets from the Portugese.”



4 Kermit and Miss Piggy

Kermit and Miss Piggy, 20th Century, American, cultural. She hogs the limelight every chance she gets, but her love springs eternal for her froggy beau. His disinterest and the cross-species problem are no deterrents to this determined pig. 3.Shah Jahan and Arjumand Bann Begum

Shah Jahan and Arjumand Bann Begum, 17th Century, Indian, historical. Consumed with sorrow when his beloved wife died at age 39 giving birth to their 14th child, he commissioned the Taj Mahal to be built in her memory. His son later imprisoned him and he spent the rest of his life staring out the window of his room at the Taj, pining for Arjumand.

2.Peter Abelard


Peter Abelard and Heloise, 12th Century, French, historical. Theologian and lecturer Abelard was 17-year-old Heloise’s teacher. They secretly married, but her uncle found out and had him castrated. Too late — she had a son. Separated by their families and the church, she entered a convent, he became a monk, and their love letters still exist. They are buried together in Paris.

1.Romeo and Juliet

Romeo and Juliet, 16th Century, English, literary. Star-crossed lovers immortalized in Shakespeare’s 1596 play. With Romeo dead, Juliet takes her own life rather than live without her young husband.

Mti unaotoa damu nchini India

Mti huu unajulikana kama ‘The Dragon’s Blood tree ni mti ambao unafananishwa na kundi la miti iliyopo katika visiwa vinne vilivyopo Bahari ya India. Mti huu unatoa juisi ambayo inaitwa Dragon’s Blood ambayo imekuwa ikitumiwa kama dawa ya magonjwa Mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuondoa mabaya, kumkinga mtu na kuongeza mapenzi.

Haya basi wanaotafuta limbwata kazi kwenu.

Jinsi ya kuutumia sasa ndo sijajua nitatafuta njia ya kuutumia nitawaandikia.



Huu ndo unga wa mti huu


Jamani si nikapata Gonjwa!


Haaa ni Gonjwa la macho bwana wengi walikuwa wameshaanza kushtuka gonjwa gani?
Hivi mnaijua dawa ya gonjwa hili la Red Eyes ni maji ya majani ya chai, povu la sabuni au mkojo wako mwenyewe.

Jinsi ya kutumia:
Chukua kiasi cha majani ya chai changanya na maji kisha chemsha mpaka yabadirike na kuwa chai lakini usichuje. Baada ya kufanya hivyo yaache yapoe kidogo yabaki vuguvugu kisha nawia katikati ya macho kwenye mboni, nakupa siku tatu tu utaona matokeo.

Njia nyingine ni kuweka povu jingi katika macho husaidia pia.

Njia ya mwisho ni mkojo wako mwenyewe kama unaweza unachukua kiasi cha matone na kunyunyizia utapona mara moja.
Niliona niwafahamishe tiba hii kwani gonjwa hili limetanda sasa..mmesikia akina Nasra na Kambili? najua mmejibu kimoyomoyo hata kama sijawasikia

Wednesday, May 19, 2010

Cute Baby I hope 2 get very soon, God Bless Me!

Msichoke nawaletea vipande vipande tu mpaka itatimia

Hii ni video nyingine ya Marichoy na Migel inasisimua

Hii ni video nyingine ya Marichoy na Migel inasisimua

Tunaendelea kuichambua Tamthilia ya Dont mess with an Angel

Alipozaliwa Maria De Jesus, ‘Marichuy’, mama yake, Cecilia Velarde, aliamini kuwa mwanaye angefariki, akampeleka mtoto wake kwa mchungaji,aliyekuwa akiitwa Padre Anselmo, ambaye alimpeleka kwa watu wasiojiweza. Akiwa na miaka 15, Marichuy akatoroka na kukimbilia mtaani ambako alikwenda kuishi, huko alikuwa akifanya kila linalowezekana ili mradi tu aishi.

Miaka ikapita akiwa huko mtaani, siku moja akavamiwa na mlevi. Baada ya hapo akawa anapata ndoto mbaya na kujikuta akiwachukia wanaume.

Candelaria, mwanamke mmoja ambaye kazi yake ni Udobi anampa ofa ya kukaa nyumbani kwake na kumchukulia Marichury kama mtoto wake. Marichuy anafanikiwa kupata kazi nzuri na kumsaidia Candelaria.

Siku moja, Marichuy anasababisha fujo na kupelekwa mahakamani ambapo anakwenda kukutana na Jaji ambaye ni baba yake wa Damu, (Ingawa hakuna kati yao ambaye aliujua ukweli), baba huyo akataka kumpeleka Jela.

Kwa upande mwingine Juan Miguel San Roman, ambaye alifanikiwa kuokoka katika ajali ya ndege , hakuwa akimpenda mke wake Viviana, anaamini kuwa Marichuy ni msichana asiyekuwa na tatizo.

Hata hivyo Viviana anakuwa mzima anaamua kuishi maisha ya starehe bila kuifahamisha familia yake kuwa yuko hai.

Marichuy anasaidiwa na mwanasaikolojia ambaye ni Juan Miguel San Roman, ambaye anataka kuona mazuri kwa Marichuy.

Marichuy anaachiwa huru kwa dhamana ya Juan Miguel na akapanga mpango wa kuishi naye nyumbani kwake pamoja na mtoto wake, Mayita, mama mkwe wake, Onelia, na dada yake ,Rosio.

Wakati Marichuy akiwa kwenye nyumba ya Migel wakajikuta wamekuwa wapenzi. Lakini Juan Miguel anaamua kumpeleka Marichuy kwenye nyumba ya Velarde ili kulikuza penzi lao.

Estefania yeye anamchukia Marichuy kwasababu yeye pia anampenda Juan Miguel. Estefania na shangazi yake, Isabella, wanagundua kuwa Marichuy ni mtoto wa Velardes, wanamfanyia mbaya Marichuy na kumfanya aonekane mwizi ambaye alimuibia Velardes.

Cecilia anawaonya Estefania na Marichuy. Hata hivyo Estefania anafanikiwa kuanzisha uhusiano na Juan Miguel, kitendo kinachomtia wivu Marichuy.

Baada ya Patricio kuupata uongo wa Marichuy na tabia zake, Marichuy anaamua kumwambia Juan Miguel kwamba anataka kuishi na yeye, kwasababu hataki kukaa na Velardes.

Juan Miguel anakubari maombi ya Marichuy na kumchukua wakaishi pamoja.. je watu hawa watakuwa mke na mume?

Juan Miguel anagundua kuwa yeye ndio alimvamia Marichuy alipokuwa mdogo lakini Marichuy anashindwa kutambua ni jinsi gani ilitokea. Pale Juan Miguel alipoanza kumuepuka akihisi makosa yake na huenda Marichuy akamgundua, Marichury akaanza kudhani huenda Juan Miguel anamchukia, ambapo alimua kuwambia kuwa anampenda.

Juan Miguel anapanga mpango wa kumuoa.. Lakini anashindwa atafanyaje kwani tatizo ni lile alilowahi kufamfanyia alipokuwa mdogo.

Padre Anselmo na Eduardo (rafiki wa kuaminika wa Juan Miguel ) wanamuonya Juan Miguel amwambie kumwambia marichuy kabla hajamuoa kuwa yeye ndio aliyemvamia wakati akiwa mtoto lakini Miguel akahofia huenda akaharibu mapenzi yao Marichuy.

Wakaamua kufunga ndoa na kwenda kwenye fungate la maana.

Asubuhi Marichuy anapoamka anaamkia kwenye ndoto akiwa amegundua kuwa mbakaji wake ni Juan Miguel.


Miguel akamuomba msamaha kwa kitendo kile lakini hakukubari kutoa msamaha na kuamua kurudi kuishi na Candelaria.

Siku chache baada ya tukio, Juan Miguel anatembelea chama kimoja na huko anagundua mgonjwa mwingine. Kwa wasiwasi mkumbwa, akamuona mke wake ambaye alitakiwa kuwa mfu. Kwa wakati huo,akachukua jukumu la kujua kilichotokea kwa mkewe na kumsaidia kurudi katika hali yake ya kawaida.

Je itakuwaje kwa Marichuy atamsamehe Miguel au atamrudua mke wake…Hii ni

Intro ya Tamthilia muendelezo kamili Utaanza wiki ijayo…

Harufu zinazosaidia kuwa na kumbukumbu, nguvu na mood nzuri ni kama zifuatazo:


Harufu za matunda ya aina mbalimbali yapatayo tisa husaidia kuimarisha afya yako ikiwa ni pamoja na kukufanya ujisikie vizuri, leo nitaongelea harufu tatu kwa kuanzia ambazo ni tiba tosha kwa hayo niliyoyataja hapo juu
Harufu ya Tofaa la kijani ‘Green Apple’
Harufu ya tunda hili inaweza kukusaidia kupata hisia za kimapenzi na kukuweka katika hali ya furaha wakati wote, harufu hii imethibitishwa na Alan Hirsch, mkurugenzi wa utafiti wa harufu na ladha wa huko Chicago.
Mtafiti huyo anayataja matunda mengine kuwa ni banana, na piripiri manga.


***
Vuta harufu: ya chenza au Mrujuani
Kwa wenzetu waaustria, wamejifunza kuvuta harufu ya chenza kabla ya kufanya chochote na vile vile mrujuani kabla ya kufanya chochote..
Harufu hizi huwasaidia kuondoa wasiwasi pamoja kuwatuliza kama wako katika hali mbaya ya mwili kama woga na kutojisikia huru.
Jaribu kufanya hivi: Chukua kiasi kidogo cha tone la mafuta ya mrujuani paka usoni na pakaa wakati unaenda kazini kwa wale wanaofanya kazi itaondoa ‘stress’ zote na utaishi kwa amani.
Wiki ijayo nitaelezea harufu nyingine nzuri zinazoweza kuimarisha afya yako.
Harufu nyingine nzuri ni Chokolate, hii husaidia kuleta hisia za mapenzi, jamani vitu hivi watu wanavidharau lakini vina ukweli emu jaribuni muone... ni taaaaaaaaamu. harufu sasa usiseme inasisimua

Wasomaji wa Tiba Asilia




Ndugu wasomaji wa Tiba Asilia, nimekuwa nikipata sms zenu na wengine mmekuwa mkinipigia mkitaka bidhaa zangu kifupi ni kwamba najiandaa kufungua duka eneo la magomeni kwa ajili ya kuwauzia bidhaa hizi lakini kwa sasa ukinitafuta naziuzia mikononi.

kwa wale wanaotembelea mtandao huu ukitaka kuperuzi zaidi angalia kulia kwako utakuta neno limeandikwa Natural Remedies hapo unaweza kupata Tip za tiba asilia, wengi wenu mmekuwa mkishindwa kutambua jinsi ya kuzisoma humu.

Msichoke jamani, wakati mwingine nashindwa kupokea simu kwasababu ya kubanwa na kazi lakini nawaheshimu sana na msiache kunisoma kwenye Amani na Risasi

Jamani wanaburudika na slow Jam


Raha kweli ukipata rafiki mnayepatana, hawa wameamua kupata kiburudisho cha nyimbo, sijui ni nyimbo gani jamani nawatamani...

Jamani mbinu za biashara ni nyingi lol



Mwenye Supermarket kabuni mbinu yake ya kumletea wateja kama hivi anastahili sifa jamani, pesa zinatafutwa kwa tabu.

Thursday, May 6, 2010

Asha Baraka na Sister Doi wakiteta jambo

Jamani kijacho kaja, anaitwa Precious

Imelda alikuwa mama Kijacho sasa, anaitwa mama Precious si mnamuona jamani
Precious na mama yake katika pozi,lakini amesinzia jamani
wakaamua kutoa pozi la kusimama
kama kawa mama p, Katoa mimachoo...
Si namimi Sister Doi 'nikaplactize' kwani nami niko mbioni namuomba mungu jamani
Hope Siku moja nami nita 'own' kama huyuuuuuuuuuuuuuuuuuu

Wanachama nyumbani kwa Natasha

Mariam na Devotha baada ya kupata mlo
Katibu bi Angel akiwa ameshikilia pesa kwa ajili ya kukusanya kuwakabidhi Monalisa na Natasha
Mwekahazina au mhasibu mama Dotnatha akiweka kumbukumbu kwenye daftari
Mamaa Devotha akijiandaa kupakua mlo hapo nyumbani kwa Natasha
Hapa ndo keshafunua sasa kwa ajili ya kujisevia
Hapa keshapata mlo tayari kapumzika kwa raha zake
Sister Doi na Natasha wakipiga gumzo baada ya mlo
Hapa kuna mtu katuchekesha ndio maana meno nje
Da Jen katika pozi badaa ya kupata mlo, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kujichana
Mamaa Loraa naye alikuwepo kwa Natasha kama mwanachama na mshauri katika chama
Mona na Eva wa Dude wakiwa katika pozi
Hapa na Dude aliamua kuingia katika picha ya pamoja
Baada ya kubadirishana ya hapa na pale na mlo, vikaletwa vipodozi juu ya meza
Mona alishtukia namfotoa si akanigeukia kwani alikuwa akijiandaa kununua vipodozi.