.

.

Saturday, May 1, 2010

Jamani hapa duniani kila Mtu anaye Shost!

Huyu ni Shost wangu kwa kizungu 'Lol' anaitwa Shalom nampenda sana naye ananipenda, wengi wanao mashost saiz yao lakini mimi shost wangu ni huyu na tunaelewana sana tu! afu tumefanana emu angalia picha yangu ya udogo utanambia
Hapa nilikuwa studio mwaka 2002 nilipomaliza chuo cha uandishi na utangazaji..lakini nilinogewa na kuandika, napenda sana fani yangu wadau mpaka mwenyewe najiogopa
Hapa ni enzi za mwalimu, mimi na mama yangu na Pacha wangu Hamidu tukiwa na mdogo wetu Jamila.
Hapa nilikuwa nimenganda mama yangu kama Luba na mdogo wangu Jamila pembeni

Kitchen Paty ya Jose ndo hii kama harusi na nyie oleweni jamani ni raha

Sister doi nilikuwepo kama mpiga picha, aloo sherehe ilikuwa kabambe nami yangu inakujaaaaaa!!!
Hapa akikumbatiwa na dada yake
Madada walikuwa na sanduku kwa ajili ya mdogo wao
Madada,Mgeni na Jovita baada ya kutoa sanduku kwa mdogo wao
Hapa wakisasambua sanduku lao
Msasambuo unaendelea
Hapa ndo sanduku linafunguliwa
Hapo sanduku linaandaliwa na Dada yake Jovina
Jovita amewakumbatia ma lol wake waliokuwepo kumfuta jasho

Hapa ma lol wa Jovita wakimfuta jasho
Jose na mpambe wake baada ya kuserebuka sasa ni kufutwa jasho
Dada zake Jose, Jovita na Jovina wakiserebuka
Jose mwenyewe na wageni waalikwa na dada yake wakiserebuka
Mgeni Hassan naye alikuwepo akijiandaa kuchambua kama karanga kama Saida, na yeye ni wa huko huko kwetu..Kanyigoooo kwa akina Mpoki
Jose akichambua kama karanga, alikuwa anaona watu wanamchelewesha
Kuchambua kama karanga kunaendelea
Jovita naye alikuwa akijaribu kuchambua lakini baado, ntampa mafunzo siku moja
Jose akijiandaa kukata keki yake ambayo ilikuwa ni sufuria la ugari ukiwa kwenye mafiga
Keki iliwavutia wengi siku hiyo, unajua Bi Jose ameolewa na msukuma hivyo alitengenezewa keki yenye mfano wa sufuria la ugari ikiwa kama mafunzo ya chakula wanachopendelea huko alikoolewa
Hivi ni vyombo vilivyotolewa kwa ajili ya Jose

Hii ilikuwa ni send off nitawaletea kitchen paty msichoke

Shangazi maria naye alikuwepo kusherehekea na Jose
Jamali na mke wake walikuwepo kama mnavyowaona
siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Amani na mchumba wa Jose alikuwa azaliwe siku inayofuata wakakata keki kwa pamoja, hapa wanalishana keki, ilikuwa ni furaha tupu
Madada zake Jose,Mgeni,Jovita,Koku,Jovina,Joyce, Sima na wengine wakiserebuka baada ya kutoa zawadi, walifurahi sana siku hiyo
Hapa madada wakimkumbatia kwa furaha mdogo wao Jose
Madada wakienda kumpongeza mdogo wao kama tunavyowaona
Hapa sister Doi nikiwa na kampani yangu ya siku hiyo, Mwanangu Furaha na mdogo wangu Lily
Hapa nikiwa na mwanangu Furaha
Madada wakiwa katika pozi, Jovita na Mgeni kama kawa
Keki ilikuwa ni ya asili na ilikuwa tamu ajabu
Joice na mumewe katika pozi
Madada walifurahi na mwisho wakajikuta wakilia kwa uchungu baada ya kuwakumbuka wazazi wao ambao mungu aliwatanguliza mbele ya haki...Mungu awalaze pema peponi amina. Baada ya hapo majonzi yalikaa pembeni na sherehe ikaendelea kama kawa, madada hao ni Jovita mbele, Joice anayefuata na Sima.

Thursday, April 29, 2010

Send off ya Jose Njunwa

Hapa amepiga picha na mheshimiwa waziri mkuu mstaafu

Akijiandaa kupeleka keki kwa wakwe zake
Akielekea kukata keki


Jose akiwa na mume wake na matroni wake




Jose na ndugu zake kama tunavyowaona walikuwa katika furaha ,lakini pia walipata majonzi kwa kumbukumbu ya wazazi wao waliotangulia mbele ya haki mungu awalaze pema peponi, kwani ilikuwa ni siku ambayo hakika wangefurahi kuona sherehe ya mtoto wao



Saturday, April 17, 2010

Baada ya shughuri zote Tukafunguliwa muziki na Mama kijacho tukajumuika wote

Hawa walikuwa wakibadirishana mawazo
Jack naye aliserebuka kiaina
Mama kijacho kafurahi huyo
muziki alicheza sana tukadhani atajifungua siku hiyo, jamani ilikuwa ni furaha
Mama kijacho akifungua muziki na Johari
Hawa wakanogewa muziki na kuoneshana miguu wakilingishiana nani zaidi
Fide akisaka lumba kwa madaha na kinywaji chake
Hapa umekolea kweli kila mtu na zake staili
Hapa mama kijacho wala hakumbuki nyumbani kwani ukumbini kulimtoshereza kwa kila kitu